BRAZIL WATWAA COPA AMERICA BAADA YA KUICHAPA 3-1 PERU

Wachezaji wa Brazil wakifurahia na taji
lao la Copa America baada ya kukabidhiwa kufuatia ushindi wa 3-1 dhidi
ya Peru kwenye fainali usiku wa kuamkia leo Uwanja wa Jornalista Mario
Filho, au Maracana mjini Rio de Janeiro.
Mabao ya Brazil yalifungwa na Everton
dakika ya 15, Gabriel Jesus dakika ya 45 na ushei kabla ya kutolewa kwa
kadi nyekundu dakika ya 70 kufuatia kuonyeshwa kadi ya pili ya njano na
Richarlison kwa penalti dakika ya 90, wakati la Peru lilifungwa na Paolo
Guerrero kwa penalti pia dakika ya 44, hilo likiwa taji lao la kwanza
tangu mwaka 2007 PICHA ZAIDI SOMA HAPA
No comments:
Post a Comment