BASHIRU AWATAKA MACHINGA KUWA NA MSHIKAMANO
Na.Faustine Gimu Galafoni,Dodoma.
KATIBU Mkuu wa Chama Cha
Mapinduzi(CCM)Dkt.BASHIRU ALLI amelitaka Shirikisho la Umoja wa
wamachinga nchini Taifa (SHIUMA)kuzingatia mshikamano miongoni mwao ili
kukabili migogoro ya kiuongozi inayoweza kutokea.
Ushauri huo ni miongoni mwa mambo matatu
aliyotoa kwao baada ya SHIUMA kufika ofisini kwake jijini Dodoma
kuwasilisha pongezi zao kwa Mweyekiti wa Chama Cha Mapinduzi(CCM)dokta
JOHN MAGUFULI kwa juhudi zake anazofanya za kuwatambua shughuli
wanazofanya.
Akipongea pongezi hizo kwa niaba ya Rais
dokta MAGUFULI,dokta BASHIRU amesema pia wanapaswa kuwekeza kwenye elimu
na kutumia jasho na nguvu zao katika kuwalea watoto kwenye maadili.
Wakizungumza na waandishi wa Habari
Makao makuu CCM Taifa,viongozi wa shirikisho hilo wamesema lengo kubwa
la kufika kwao ni kumpongeza Rais MAGUFULI kwa hatua yake ya kuwapa
viitambulisho vinavyowasaidia kufanya shughuli zao bila ya bugudha.
Aidha,Mwenyekiti wa Machinga Taifa
Bw.Matondo Masanja amesema wazo La vitambulisho vya machinga ni la
machinga wenyewe hivyo wanasiasa wanapaswa kuacha kuupotosha umma kuwa
ni la Rais Magufuli bali yeye alipokea mawazo ya machinga hao la
kuwapatia vitambulisho na kulitekeleza mara moja ilikuwaondolea kero
mbalimbali.
SHIUMA kwa sasa ina wanachama katika mikoa 16 ya tanznaia Bara lengo lake likiwa ni kufika katika mikoa yote nchini.
No comments:
Post a Comment