WAZIRI WA AFYA HAMAD RASHID MOHAMED AHUTUBIA SIKU YA WACHANGIAJI DAMU DUNIANI MWANAKWEREKWE ZANZIBAR
Wafanyakazi wa Kitengo cha Damu Salama
Hasina Khamis Masoud na Ussi Bakar Mohamed wakiwa katika kazi ya
kuwapima Damu wananchi mbalimbali waliojitokeza katika siku ya Wachangia
Damu Duniani(WORLD BLOOD DONOR DAY)iliofanyika Uwanja wa Mwanakwerekwe
Sokoni mjini Zanzibar.
Waziri wa Afya Hamad Rashid Mohamed
akimkabidhi zawadi Mchangiaji Bora wa Damu Rashid Adam Mtawa ambae
anadamu Group ‘O’Nagative katika siku ya Wachangia Damu Duniani(WORLD
BLOOD DONOR DAY)iliofanyika Uwanja wa Mwanakwerekwe Sokoni mjini
Zanzibar.
Waziri wa Afya Hamad Rashid Mohamed
akitoa hotuba katika hafla ya siku ya Wachangia Damu Duniani(WORLD BLOOD
DONOR DAY)iliofanyika Uwanja wa Mwanakwerekwe Sokoni mjini Zanzibar.
Wananchi mbalimbali waliojitokeza
kuchangia Damu katika siku ya Wachangia Damu Duniani(WORLD BLOOD DONOR
DAY)iliofanyika Uwanja wa Mwanakwerekwe Sokoni mjini Zanzibar.
PICHA NA YUSSUF SIMAI/MAELEZO ZANZIBAR.
……………………
Na Khadija Khamis – Maelezo Zanzibar
Waziri wa Afya Hamad Rashid Mohamed
amewataka wananchi waongeze juhudi ya kuchangia damu ili kuokoa maisha
kwa wagonjwa aliokuwa hatarini ambao wanahitajika kusaidiwa damu
kutokana na matatizo mbali mbali.
Hayo aliyasema huko katika Uwanja wa
Mwanakwerekwe Sokoni Wilaya ya Magharibi B Unguja wakati wa Sherehe ya
Kuadhimisha siku ya uchangiaji damu duniani .
Alisema wananchi wenye moyo wa kuchangia
damu kwa hiyari huokoa maisha ya watu wengi ambao wanahitaji huduma ya
kusaidiwa damu wakiwemo mama wajawazito na waliojifungua ni zaidi ya
asilimia 75 ,wahanga wa ajali pamoja na wagonjwa wanaofanyiwa upasuaji
.
“Damu ni uhai bila ya damu huna uhai
huwezi kufanya kazi kama huna damu ya kutosha pia huwezi juwa wakati
gani utapata tatizo. “alisema Waziri wa Afya
Aidha alisema ukaguzi unahitajika katika
sehemu zote zinazohifadhiwa damu ili kuhakikisha damu iliyopo ipo
katika hali ya usalama na inatumika ipasavyo bila ya kukaa hadi
kuharibika.
Alifahamisha kuwa utowaji wa damu kwa
wananchi kumesaidia kuepua matatizo mbali mbali ya Maradhi hasa magonjwa
ya ini ambayo yameonekana kwa baadhi ya wananchi ambao walikuwa bado
hawajajibaini na kuweza kupatiwa huduma za tiba mapema .
Alisema takwimu zinahitajika kwa kila
wilaya kuweza kujuwa kiasi gani cha mahitaji ya damu ambayo yanahitajika
ili kuweza kujipanga kwa mujibu wa mahitaji yaliopo.
Pia aliwashukuru wananchi kwa uwelewa wa
kujitokeza katika kuchangia damu kwani kila siku mahitaji ya damu
yanahitajika kuongezeka kutokana na ongezeko la idadi ya watu .
Hata hivyo alitoa shukurani kwa wananchi
mbali mbali Jumuiya pamoja na Taasisi za Serikali ikiwemo Vikosi vya
Serikali ya Mapinduzi Zanzibar na Vikosi vya ulinzi na usalama,sehemu za
ibada Msikitini pamoja na Kanisani.
Nae Mkuu wa Wilaya Magharibi B Kapteni
Silima Haji Haji alipongeza jitihada zilizochukuliwa za uhamasishaji
wananchi pamoja na jumuiya mbali mbali ili kujitokeza kwa wingi kwa
kuitika wito huo wa kuchangia damu zao .
Aidha alisema kufanya hivyo ni kusaidia
kuokoa maisha ya watu wengi ambao wanapata matatizo mbali mbali ya
kiafya ikiwemo wahanga wa ajali .
Kaimu Meneja wa mpango wa damu salama
Uchangiaji Omar Juma Kidawa alisema wataendelea kuwahamasisha wananchi
katika sehemu mbali mbali ili hakikisha uchangiaji unaongezeka kulingana
na mahitaji ya wananchi .
Alisema kila siku idadi ya wachangiaji
inazidi kuongezeka kuanzia Januari mosi hadi sasa imeshapatikana damu
unit 6954 jambo ambalo linatia moyo sana kila siku idadi inaengezeka ya
uchangiaji kwa wananchi.
Meneja Mstaafu wa kuchangiaji damu
Mwanakheir Mahamoud aliahidi kuwa sambamba katika kuhamasisha watu
kuchangia damu kwani ni suala muhimu ambalo linaokoa wengi kwa kuweza
kuchangiwa damu salama .
Katika Sherehe hiyo ya Uchangiaji Damu
Duniani zawadi mbali mbali zimetolewa kwa Wananchi Jumuiya, Taasisi
pamoja na Nyumba za Ibada kwa kuwa wachangiaji bora
No comments:
Post a Comment