TIBA RADIOLOJIA YAWAFIKIA WAGONJWA WA FIGO,KINA MAMA WENYE UVIMBE KWENYE KIZAZI
Mtaalam wa Tiba Radiolojia
(Interventional Radiology) wa Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH), Dkt.
Erick Mbuguje (mwenye kofia ya bluu) na wenzake wa MNH wakifuatilia
jinsi mtaalam wa Tiba Radiolojia kutoka Marekani, Dkt. Michelle Maneeveseanavyomwekea mgonjwa wa figo mpira maalum kwenye mshipa mkubwa wa damu (permanent catheter insertions) ambao unamsaidia mgonjwa kusafisha damu (renal dialysis).
…………………
Hospitali
ya Taifa Muhimbili (MNH) imeanzisha huduma mpya ya kutibu uvimbe
kwenye kizazi (uterine fibroids) kwa kutumia njia ya kisasa yaTiba
Radiolojia (interventional radiology).
Pia, MNH imeanzisha huduma mpya nyingine ya kuweka mipira maalum kwenye mshipa mkubwa wa damu (permanent catheter insertions) kwawagonjwa wa figo ambao wapo kwenye mfumo wa kusafisha damu (renal dialysis) au kwa wagonjwa wanaopatiwa tiba ya saratani.
Wataalam
wa MNH kwa kushirikiana na Chuo Kikuu cha Yale na vyuo shiriki (kama
Emory, Dartmouth) vya nchini Marekani wako kwenye programu maalum ya
mafunzo ya tiba Radiolojia tangu Octoba mwaka 2018 hospitalini hapa.
Akizungumza
na waandishi wa habari leo, Daktari Bingwa wa Tiba Radiolojia wa MNH,
Dkt. Flora Lwakatare amesema mgonjwa mwenye uvimbe kwenye kizazi
anaingiziwa mpira wenye chembechembe maalum kwenye mishipa ya damu na
kwenda kuziba mishipa inayopeleka damu kwenye uvimbe.
“Baada
ya mishipa kuziba uvimbe unakosa damu au chakula chake na hivyo
kusinyaa na kufa kabisa. Hivyo basi mama mwenye uvimbe kwenye kizazi
endapo anapatiwa tiba hii hakuna haja ya kumfanyia upasuaji kubwa wa
kuondoa uvimbe,” amesema Dkt. Lwakatare.
Dkt
Lwakatare amesema faida ya kutumia njia hii ya kisasa, inamsaidia
mgonjwa kutofanyiwa upasuaji mkubwa na pia inampunguzia gharama za
matibabu na kuondoa hatari yoyote kwa mgonjwa aliyefanyiwa upasuaji
mkubwa.
Akizungumzia huduma nyingine ya kuweka mipira maalum kwenye mshipa mkubwa wa damukwawagonjwa
wanaosumbuliwa na figo, Dkt Lwakatare amesema huduma hii inawanufaisha
wagonjwa wa figo ambao wako kwenye mfumo wa kusafisha damu (renal dialysis) au wanaopatiwa tiba ya saratani.
Amesema
tiba hii inaondoa usumbufu wa kutumia mishipa midogo ya mikononi ambayo
mara nyingi ni ngumu kupatikana hasa kama inatumika mara kwa mara na
kwa muda mrefu.
“Tiba
hii inafaida kubwa kwa kuwa inawezesha kuepeuka upasuaji mkubwa ambao
una vihatarishi (risk), kuepeuka mgonjwa kukaa hopsitali kwa muda mrefu
na wanaofanyiwa tiba radiolojia mara nyingi wanaweza kurudi nyumbani
siku hiyo hiyo, hivyo inapunguza gharama kwa mgonjwa na Hospitali kwa
ujumla,” amesema.
Hivyo
kujengewa uwezo kwa watalaam wa ndani itasadia kwa kiwango kikubwa
kukuza huduma hii hapa nchini ambapo watalaam kutoka Hospitali za hapa
nchini watapata fursa ya kujifunza kwa gharama nafuu na kuongeza idadi
ya watoa huduma mikoani.
Naye
Daktari Bingwa wa Tiba Radiolojia wa Hospitali ya Chuo Kikuu cha Emory
nchini Marekani, Dkt. Janice Newsome amesema tiba radiolojia inahitaji
ubunifu na kutoa huduma kwa kushirikiana.
Dkt.
Janice Newsome amesema wametoa mafunzo ya kutoa huduma ya tiba
radiolojia kwa wataalam wa MNH na kwamba wao wamejifunza mambo
mbalimbali kupitia wataalam wetu.
“Kuwekeza kwa wataalam ni jambo muhimu na zuri kwa kuwa kazi ya kutoa huduma inahitaji kushirikiana,” amesema Dkt. Newsome.
Katika
mafunzo haya ya awamu ya nne, wataalam 13 wa MNH wakiwamo madaktari,
wauguzi na mafundi sanifu wamepatiwa mafunzo sambamba na kutoa huduma ya
matibabu kwa wagonjwa mbalimbali.
Mafunzo
na huduma za tiba radiolojia zinazotolewa MNH ni mfululizo wa programu
mbalimbali za tiba radiolojia yayolianza Novemba 2017 ili kujenga uwezo
kwa wataalam wa MNH. Tangu kuanzishwa kwa huduma hii, wagonjwa 339
wamepatiwa huduma ya kibingwa ya tiba radiolojia na wengi ni wagonjwa
wenye uvimbe kinywani.
No comments:
Post a Comment