Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto Ummy Mwalimu,akizungumza wakati wa uzinduzi wa mpango mkakati wa taifa wa masikio na usikuvu leo jijini Dodoma.
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto Ummy Mwalimu,akikata utepe kuashiria uzinduzi wa mpango mkakati wa taifa wa masikio na usikuvu leo jijini Dodoma.Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto Ummy Mwalimu,akizungumza wakati wa uzinduzi wa mpango mkakati wa taifa wa masikio na usikuvu leo jijini Dodoma.
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto Ummy Mwalimu,akiwa ameshikiria kitabua akiwaonesha wananchi (hawapo pichani) mara baada ya kuzindua mpango mkakati wa taifa wa masikio na usikuvu leo jijini Dodoma.
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto Ummy Mwalimu,akiwa katika picha ya pamoja baada ya kuzindua mpango mkakati wa taifa wa masikio na usikuvu leo jijini Dodoma.
…………………
Na.Alex Sonna,Dodoma
Serikali imezindua mpango mkakati wa taifa wa masikio na usikuvu ambao utasaidia kupeleka huduma za matibabu ya masikio, pua na koo katika ngazi za chini ili kukabilina na tatizo la usikivu kwa wanachi.
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto Ummy Mwalimu,akizindua mpango huo jijini Dodoma amesema kuwa ni lazima watumishi katika ngazi za wilaya ndani ya miezi sita ijayo, wajengewe uwezo ili huduma hizo zipatikane katika ngazi za chini na siyo kusubiri kwenda Muhimbili.
Aidha Waziri Ummy pia amezindua kambi ya matibabu pamoja na huduma ya uchunguzi wa afya ya sikio unaotolewa na Taasisi ya Starkey hearing Foundation ya nchini Marekani kwa kushirikiana na serikali ya Tanzania.
Hata hivyo amesema kuwa pamoja na Serikali kukosa takwimu sahihi za tatizo la usiku nchini lakini pamekuwepo na tafiti ndogondogo ambazo zimekuwa zinafanywa na wadau mbalimbali wa masula hayo.
“Katika tafiti hizo zinaonyesha kuwa asilima 3 ya mwanafunzi
wanamatatizo ya kusikia na usikuvu hii inamaanisha kuwa kati ya watoto
100 watatu wanamatatizo ya usikivu”amesema Mhe.Ummy
No comments:
Post a Comment