ALLY ALLY ASAINI YANGA MKATABA WA MIAKA MIWILI
Beki kiraka wa timu ya KMC, Ally Ally ‘Mwarabu’ amejiunga na mabingwa
wa kihistori Yanga kwa kusaini mkataba wa miaka miwili kama mchezaji
huru baada ya kumaliza mkataba wake na timu ya KMC
Ally amekuwa bora ndani ya KMC hali iliyomvutia Kocha wa Yanga,
Mwinyi Zahera na kuacha maagizo kwamba naye aongezwe kwa wachezaji wa
ndani.
Makamu Mwenyekiti wa Yanga, Fredirick Mwakalebela amesema kuwa
mipango ya usajili inaendelea kwa sasa kwa wachezaji wa ndani kwani wale
wa kigeni wamekamilisha maagizo ya mwalimu kwa asilimia 90.
No comments:
Post a Comment