Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Mh. Joachim Wangabo (mbele) akikagua ujenzi wa jengo la Wazazi katika hospitali mpya ya wilaya ya Nkasi
Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Mh. Joachim Wangabo
Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Mh. Joachim
Wangabo (wa pili toka kulia) akiongea mawili amatatu na Mkuu wa Wilaya
ya Nkasi Mh. Said Mtanda (kulia) wakati wakiendelea na ukaguzi wa ujenzi
wa hospitali ya Wilaya ya Nkasi.
*************************************
Mkuu wa mkoa wa Rukwa mh.
Joachim Wangabo amesikitishwa na uvivu wa kutofanya kazi kwa vijana wa
kiume katika mkoa hali inayopelekea miradi mingi inayotekelezwa na
serikali katika mkoa huo kwa kutumia force account inafanywa na vijana
wanaotoka nje ya mkoa huo jambo ambalo sio madhumuni ya serikali ya
awamu tano.
Amesema kuwa lengo la ujenzi kwa
kutumia force account ni kuhakikisha kwamba wananchi wa maeneo husika
wanapata manufaa ya ujenzi ule na kufanya ujenzi huo kuwa ni wa kwao na
kujivunia kwamba walishiriki tangu mwanzo wa ujenzi huo kuanzia ngazi ya
songambele ya kuchimba msingi hadi kumalizika kwa majengo hayo
“Watu wameshiriki kweny songambele
hapa lakini baadae tunapotafuta vibarua wa kufanya kazi, mtu anafanya
siku mbili, siku tatu akipewa malipo yake anapotea, Uvivu, sasa hii
tabia ya uvivu hii ndio ambayo ningependa kutoa wito kwa wananchi wangu
ndani ya mkoa wa Rukwa kuwa waache uvivu, mbona kuna mabinti na kina
mama wanachapa kazi kule, hawakimbii wanapiga kokoto na wako wengi,
lakini vijana wa kiume wanataka kupiga draft, kufanya vitu vyepesi
vyepesi, hii tabia ningewaasa waiache,” alisema
Ameongeza kuwa kwa kufanya hivyo
miradi hivyo wanakosa umiliki wa miradi hiyo na kuiona ni miradi
isiyowahusu na hivyo kuwataka wananchi kujitokeza katika ufundi na
vibarua ili kufanye kazi na kujipatia kipato na kuacha uvivu.
Ameyasema hayo alipotembelea
ujenzi wa hospitali ya Wilaya ya Nkasi inayojengwa katika mji mdogo wa
Namanyere wilayani humo akiongozana na kamati ya ulinzi na usalama ya
mkoa pamoja na wataalamu kutoka katika ofisi ya mkuu wa mkoa.
Katika ziara hiyo Mh. Wangabo
amepongeza hatua iliyofikiwa katika ujenzi huo unaoendelea huku majengo
yote saba ya hospitali hiyo yakiwa yamefikia katika hatua ya kupaua na
kuzingatia ubora katika ujenzi huo huku vifaa vyote kwaajili ya ujenzi
huo vikiwa tayari vimeshanunuliwa na kuwaasa kuwa hadi kufikia tarehe
30.6.2019 wahakikishe mafundi wanakabidhi majengo hayo kwaajili ya
kuanza kutumika.
Mmoja wa vibarua anaetokea mkoa wa
shinyanga Joseph James kwa niaba ya wenzie alisema kuwa tangu wafike
hapo wamekuwa wakilipwa vizuri na wanaona kuwa kazi zinakwenda sawa na
hawana malalamiko yoyote huku fundi wao mkuu katika jengo la maabara
alikiri kuwa vibarua wake anawatoa mkoa wa shinyanga na kuwa vijana
waliopo katika wilaya ya Nkasi ni wavivu na walikuwa wakirudisha nyuma
kasi ya kazi.
Awali akitoa taarifa ya maendeleo
ya ujenzi wa hospitali hiyo Mkuu wa Wilaya ya Nkasi Mh. Said Mtanda
alisema kuwa ujenzi huo unakwenda kwa awamu tatu na hadi kufikia tarehe
15.6.2019 awamu ya kwanza itakuwa imeisha na awamu ya pili ya kupaka
majengo rangi pamoja na kuweka fremu za milango na madirisha tayari
imeshaanza kufanyika na awamu ya mwisho ni kuweka marumaru kwenye
majengo yote hivyo hadi kufikia tarehe 30.6.2019 ujenzi huo utakuwa
umekamilika.
“Kwa zote hadi sasa tumeshatumia
kama shilingi bilioni 1.15 na mpaka jana kweny akaunti tuna kama
shilingi milioni 351 ambazo matarajio yetu ni kwamba zitakidhi shughuli
za mradi kwasababu kwa upande wa mafundi wote wameshalipwa haki zao kitu
ambaco kimebakia katika kununua ni masuala ya marumaru na kulipia
aluminiam ya vioo na kumalizia kuwalipa mafundi wakaofanya kazi awamu ya
pili, matarajio yetu fedha hiyo itakidhi mahitaji hayo,” Alimalizia.
No comments:
Post a Comment