Na Mwandishi Wetu
RAIS Mstaafu wa Awamu ya Nne, Jakaya Mrisho Kikwete amewaasa viongozi
nchini kutotumia ushabiki wao wa mpira kukandamiza timu pinzani.
Jakaya, maarufu kama JK ameyasema hayo wakati akizungumza kwenye tamasha
maalum la kuchangia klabu ya Yanga Jumamosi ukumbi wa Diamond Jubilee
lililojulikana kama “Kubwa Kuliko”.
“Unatumia ushabiki wako wa mpira kukandamiza timu nyingine,” alisema
Rais Mstaafu Jakaya Kikwete akitoa angalizo kwa viongozi wa Serikali.
Pamoja na hayo, Rais Kikwete klabu nchini
ziwekeze kwenye soka ya vijana ili kuinua vipaji kuliko kugombea
wachezaji wa kigeni, kwani kufanya hivyo ni kuawafaidishia wenzao.
Rais Mstaafu Kikwete pia alisema Yanga kwa sasa imepoteza makali yake kiasi kwamba inazidiwa na mahasimu wao wa jadi, Simba.
Kauli hiyo iliungwa mkono na Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania, Kassim Majaliwa ambaye alisema klabu hiyo inatakiwa
kujiimarisha tena ili kurejesha ushindani katika soka nchini; “Bila
Yanga imara, hakuna Simba imara,” alisema Majaliwa.
Pamoja na hayo, Waziri Mkuu alitoa Sh. Milioni 10 kama mchango wake
kwenye harambee ya Yanga, huku Kikwete akichangia Sh. Milkioni 5.
No comments:
Post a Comment