WAZIRI BASHUNGWA ATAJA VIPAUMBELE VYAKE WIZARA YA VIWANDA NA BIASHARA
Waziri wa Viwanda na Biashara Innocent
Bashungwa, akizungumza na wanahabari (hawapo pichani) muda mfupi baada
ya kufanya kikao na wakurugenzi wa taasisi 16 na bodi zilizochini ya
wizara hiyo, jijini Dodoma.
Mwenyekiti wa Bodi ya Tume ya ushindani
Hamfrey Mosha, akizungumza na wanahabari mda mfupi baada ya kufanya
kikao na Waziri wa Viwanda na Biashara Innocent Bashungwa jijini
Dodoma.
Kaimu Mtendaji Mkuu wa wakala wa usajili
wa biashara na leseni, Emanuel Kakwesi, akizungumza na wanahabari mda
mfupi baada ya kikao cha wakuu wa taasisi na bodi zilizochini ya Wizara
hiyo na Waziri wa Viwanda na Biashara Innocent Bashungwa jijini Dodoma.
Picha na Mpiga Picha Wetu.
……………………..
Na.Alex Sonna, Dodoma
WAZIRI wa viwanda na biashara Innocent
Bashungwa amezitaka taasisi zilizochini ya wizara hiyo kutengeneza
mipango wezeshi ambayo ambayo itasaidia kututoa hapa tulipo na
kutufikisha katika uchumi wa viwanda, mipango ambayo haitakuwa kandamizi
kwa wawekezaji.
Sambamba na kujenga uhusiano mzuri baina
ya taasisi hizo na wenye viwanda, wafanya biashara ili kwa pamoja kuona
changamoto ambazo zinawakabiri wafanyabiashara ambazo ni kikwazo
kufikia malengo.
Ameyasema hayo jijini Dodoma wakati wa
kikao kazi baina ya wakuu wa taasisi kumi na sita (16) pamoja na bodi
zilizochini ya wizara hiyo, waliokutana kwa siku mbili Dodoma kujadili
mbalimbali na namna ya kufikia walengo ya serikali.
Amezitaka taasisi hizo kuja na mbinu
ambazo zitasaidia kuinua sekta hiyo bila kuathiri wawekezaji na kukaa
na wawekezaji kubaini changamoto mbalimbali ambazo wanakabiliana nazo
katika kutekeleza majukumu yao.
“Lengo la kikao hiki ni kukaa na taasisi
zetu ili kuona namna bora ya kufikia malengo tuliyojiwekea na mambo
ambayo ni kikwazo katika kutekeleza, sasa niwatake taasisi msiwe
kikwazo kwa wawekezaji, mtengeneze mipango ambayo itasaidia kututoa hapa
tulipo na mipango ambayo haitakuwa kikwazo kwa wawekezaji” amesema
Bashungwa.
Ametolea mfano kwa shirika la viwanda
Tanzania TBS kuhakikisha bidhaa zinazozalishwa kuwa na viwango, pia
katika kudhibiti viwango wahakikishe hawaathiri wala kuchelewesha
shughuri za mwekezaji.
Amesema katika kikao ambacho Rais wa
jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Magufuli alikaa na
wafanyabiashara ikulu kilimpa mwanga namna ya kuja kufanya kazi ndani ya
wizara hiyo na atahakikisha anasimamia kikamilifu wizara hiyo.
Amesema matokeo ya kikao hicho tayari
yameanza kuonekana ambapo kodi na tozo zilizokuwa kero zimeondolewa
zaidi ya 54, amesema sambamba na hilo atahakikisha anafanya mageuzi
katika sekta hiyo.
Kwa sababu amebaini kuwa unaweza kufuta
kodi hizo lakini tatizo likabaki palepale, amesisitiza kwenye taasisi
kuimarisha mahusiano na wawekezaji na namna ya kuongea na
wafanyabiashara, linaweza kuwa sida sio kero ya kodi bali ni mahusiano
baina yao.
Amebainisha kuwa kuna haja ya
kufungamanisha sekta ya kilimo na viwanda ili kuleta matokeo chanya
katika wizara ya viwanda na biashara, amesema kuna uhusiano mkubwa baina
ya kilimo na viwanda hivyo vikifungamanishwa vinaweza leta matokeo
mazuri.
Amesema ataimarisha mahusiano na jumuiya
ambazo Tanzania ni mwana chama kama EAC na SADC ili tuweze kufaidika na
kuwa wanachama kwa sababu Tanzania inalipa ada kila mwaka ni lazima ione
matokeo yake na hasa katika sekta ya uwekezaji.
Kwa upande wake mwenyekiti wa bodi ya
tume ya ushindani Hamfrey Mosha, amesema kikao hicho kilikuwa na faida
kwa sababu kimezikutanisha taasisi kumi na sita(16) zilizochini ya
wizara hiyo na kujiona kumbe wanaweza kufanya jambo ila walikosa nafasi
tu kama hiyo.
“Kikao kimekuwa kizuri taasisi zaidi ya
16 tumekutana jambo ambalo halijawahi kufanyika na kwa kikao hiki
tumejiona kumbe tunaweza kufanya jambo ndani ya wizara hii” amesema.
Amesema wao kama tume ya ushindani
wanafanya kazi kwa weredi mkubwa kwa kudhibiti bidhaa bandia kuingia
nchini kwa kuhakikisha tunakagua makontena yote yanayoingia katika
bandari zetu.
No comments:
Post a Comment