AZAKI ZATAKIWA KUWEKA MIFUMO MAKINI YA USIMAMIZI FEDHA
Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya
Uwezeshaji wa AZAKI,Bw. Francis Kiwanga,akitoa taarifa kwa mgeni rasmi
katika Uzinduzi wa wakati wa mkutano na Wakurugenzi wa Asasi pamoja na
zoezi la kusaini mikataba ya Ruzuku kwa ajiri ya utekelezaji wa miradi
Tanzania bara na Visiwani Naibu Waziri wa Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa
na Serikali za Mitaa, TAMISEMI, Mhe.Mwita Waitara.
Naibu Waziri wa Ofisi ya Rais Tawala za
Mikoa na Serikali za Mitaa, TAMISEMI, Mhe.Mwita Waitara,akitoa hotuba
katika Mkutano wa Wakurugenzi wa AZAKI na Zoezi la kusaini Mikataba ya
Ruzuku kwa ajili ya Utekelezaji wa Miradi Tanzania bara na Visiwani
katika Ukumbi wa Mikutano ya Royal Vilalage Hotel leo jijini Dodoma
Sehemu ya Wakurugenzi wa AZAKI
wakifuatilia Hotuba ya Naibu Waziri wa Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na
Serikali za Mitaa, TAMISEMI, Mhe.Mwita Waitara,wakati wa Mkutano wa
Wakurugenzi wa AZAKI na Zoezi la kusaini Mikataba ya Ruzuku kwa ajili ya
Utekelezaji wa Miradi Tanzania bara na Visiwani katika Ukumbi wa
Mikutano ya Royal Vilalage Hotel leo jijini Dodoma
Naibu Waziri wa Ofisi ya Rais Tawala za
Mikoa na Serikali za Mitaa, TAMISEMI, Mhe.Mwita Waitara,akikata utepe wa
kuashiria ufunguzi wa Mkutano wa Wakurugenzi wa AZAKI na Zoezi la
kusaini Mikataba ya Ruzuku kwa ajili ya Utekelezaji wa Miradi Tanzania
bara na Visiwani katika Ukumbi wa Mikutano ya Royal Vilalage Hotel leo
jijini Dodoma
Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya
Uwezeshaji wa AZAKI, Bw.Francis Kiwanga akisimamia baadhi ya wadau wa
AZAKI Zoezi la kusaini Mikataba ya Ruzuku kwa ajili ya Utekelezaji wa
Miradi Tanzania bara na Visiwani katika Ukumbi wa Mikutano ya Royal
Vilalage Hotel leo jijini Dodoma
Mkurugenzi wa Taasisi ya Tusonge kutoka
Moshi Bi.Aginata Rutazaa,akitoa shukrani kwa Naibu Waziri wa Ofisi ya
Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, TAMISEMI, Mhe.Mwita
Waitara,mara baada ya kuwafungulia Mkutano wa Wakurugenzi wa AZAKI na
Zoezi la kusaini Mikataba ya Ruzuku kwa ajili ya Utekelezaji wa Miradi
Tanzania bara na Visiwani katika Ukumbi wa Mikutano ya Royal Vilalage
Hotel leo jijini Dodoma
Naibu Waziri wa Ofisi ya Rais Tawala za
Mikoa na Serikali za Mitaa, TAMISEMI, Mhe.Mwita Waitara,akiwa katika
picha ya pamoja na baadhi ya washiriki na viongozi wa AZAKI baada ya
kufungua Mkutano wa Wakurugenzi wa AZAKI na Zoezi la kusaini Mikataba
ya Ruzuku kwa ajili ya Utekelezaji wa Miradi Tanzania bara na Visiwani
katika Ukumbi wa Mikutano ya Royal Vilalage Hotel leo jijini Dodoma.
Picha na Alex Mathias wa Waohurublog
………………..
Na.Alex Mathias,Dodoma
Naibu Waziri wa Ofisi ya Rais Tawala za
Mikoa na Serikali za Mitaa, TAMISEMI, Mwita Waitara, amezitaka asasi za
kiraia AZAKI, kuhakikisha zinaweka mifumo mizuri ya kusimamia fedha za
miradi ili kuhakikisha zinawanufaisha wahitaji.
Sambamba na hilo amezitaka kufanya kazi
kwa ukaribu na maafisa wa serikali za mitaa kwenye maeneo yanayotekeleza
majukumu yao na kutoa taarifa kwa halmashauri ambako miradi hiyo
inatekelezwa.
Ameyasema hayo leo Jijini Dodoma wakati
wa mkutano na Wakurugenzi wa Asasi hizo, na zoezi la kusaini mikataba ya
Ruzuku kwa ajiri ya utekelezaji wa miradi Tanzania bara na Visiwani.
Amesema wahakikishe wanaweka mifumo
mizuri ya usimamizi sahihi wa fedha za miradi wanayoitekeleza na
kuhakikisha wahusika wananufaika na wanafikiwa kufikiwa na miradi hiyo.
“Niwaombe sana hakikisheni mnafanya
matumizi sahihi ya fedha za miradi hii mnayoitekeleza na kuhakikisha
wanafuika halisi wanafikiwa na kufaidika na miradi hiyo, poa mhakikishe
mnawahusisha maafisa wa serikali za mitaa kwenye maeneo ya utekelezaji”
amesema Waitara.
Amesema Serikali inatambua mchango mkubwa
unaotolewa na asasi za kiraia katika kusukuma mbele maendeleo vijijini,
kuleta teknologia mpya na rahisi kwa wananchi na kupinga mila potofu na
kandamizi miongoni mwa jamii hasa maeneo ya pembezoni.
Amezitaka AZAKI zinapojenga uwezo kwa
wananchi wajenge pia uwezo kwa viongozi wa serikali za mitaa ili wajue
na kutekeleza majukumu yao kiufanisi kwa kupitia mafunzo mbalimbali
katika miradi hii kwa pamoja washirikiane katika kutayua changamoto
zilizopo.
Aidha amewataka AZAKI kutoa elimu kwa
vijana juu ya mikopo ya vikundi inayotolewa na serikali ili waweze
kunufaika, amesema imekuwa ikitolewa lakini vijana hawajitokezi
kuchukua mikopo hiyo na kuwaacha akina mama wakinufaika na mikopo hiyo.
Akizungumzia ruzuku kwa mwaka huu
Mkurugenzi mtendaji wa Taasisi ya uwezeshaji wa AZAKI, Francis Kiwanga
amesema kwa mwaka huu watatoa kiasi cha shilingi Bilioni 11.7, kwa
asasi za kiraia 154 ambazo zimekidhi vigezo vya kupata ruzuku hiyo ili
wakatekeleze majukumu yao.
Amesema madhumuni ya Taasisi hiyo ni
kuwekeza katika utoaji wa ruzuku kwa AZAKI na kuleta mabadiliko chanya
yanayogusa maisha ya watanzania kupitia AZAKI zao.
“Lengo hasa uwekezaji huu ni kuwajengea
uwezo wananchi kupitia AZAKI na nafasi kubwa tunatoa kwa asasi kutoka
ngazi za chini kabisa ya jamii ambapo wananchi wanabainisha matatizo yao
na kupendekeza utatuzi sisi tunawapatia nguvu ya ruzuku na pia
kuwajengea uwezo kupitia AZAKI” amesema Kiwanga.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa taasisi ya
Tusonge kutoka Moshi, Bi Aginata Rutazaa, amesema wao kama asasi za
kiraia watahakikisha wanaweka uwazi katika matumizi ya fedha hizo ili
ziweze kuleta tija kwa wahusika.
No comments:
Post a Comment