MWENYEKITI BODI CWT AKEMEA WANAOPOTOSHA HABARI KUHUSU CHAMA HICHO
MWENYEKITI wa Bodi ya wadhamini ya Chama
Cha walimu Tanzania (CWT), Bw.Clement Mswanyama,akizungumza na waandishi
wa habari (hawapo pichani) leo jijini Dodoma wakati akitoa taarifa za
chama hicho.
…………………
Na.Alex Mathias,Dodoma
MWENYEKITI wa Bodi ya wadhamini ya Chama
Cha walimu Tanzania (CWT), Clement Mswanyama,amewataka walioshindwa
katika chaguzi za uongozi wa nafasi mbalimbali katika Chama hicho kuacha
kutoa habari za kupotosha watu.
Hayo ameyasema leo jijini Dodoma
alipokuwa akitoa taarifa kwa waandishi wa habari kuhusu kichwa cha
habari kilichochapishwa katika gazeti fulani la hapa nchini kilichokuwa
kinasomeka “CWT KWAWAKA”.
Bw.Mswanyama amesema kuwa katika gazeti
hilo waandishi wake walieleza majengo na mali za CWT ,kampuni tanzu ya
CWT na TDCL na Benki ya Mwalimu (MCB) kuwa si mali ya walimu jambo
ambalo Ni uongo wenye nia ya kuchochea .
Aidha amesema kuwa katiba ya CWT toleo la
sita la mwaka 2014 inasema kuwa Mali za chama zitaandikishwa kwa jina
la Bodi ya wadhamini pia mikataba yote,hati na dhamana za fedha za chama
zote zitamilikiwa kwa jina la Bodi ya wadhamini na kuhifadhiwa kwa
katibu mkuu wa CWT.
“Tulizipata taarifa hizo za gazeti kwa
masikitiko makubwa na tukajiuliza wenzetu hao wamepata maelezo kutoka
kwanani na kwadhamira ipi” amesisitiza Bw.Mswanyama
Hata hivyo amesisitiza kuwa suala hili
tunahitaji kuhojiana nao kwa kina na ikibainika wamepotosha umma na
walimu kwa ujumla ni lazima tutachukua hatua za kisheria.
Bw.Mswanyama amelitaka gazeti hilo kuomba radhi kupitia gazeti lao na Kama wakishindwana watachukua hatua za kisheria juu yao.
” Ni kweli gazeti hilo lilinukuu ripoti
maalum ya mdhibiti na Mkaguzi mkuu wa hesabu za serikali(CAG) aliyekagua
CWT katika mwaka wa fedha 2016/2017
Amesema kuwa mpaka leo tunawahakikishia
walimu tumeyafanyia kazi kwa asilimia kubwa na tunaendelea na zoezi hilo
kwani ushauri mwingine ulihusu taratibu za kila siku za uendeshaji wa
Chama na matumizi ya Mali za fedha za chama.
Kwa upande mwingine Bw.Mswanyama ametolea
ufafanuzi kuhusu Teachers Development Co.Ltd (TDCL) amesema kuwa
kampuni ambayo ilianzishwa na CWT mahususi kwa ajili ya kusimamia
uwekezaji unaofanywa ndani ya Chama.
Amefafanua kuwa CAG alipofanya ukaguzi
Maalum ndani ya CWT alibaini kuwa kampuni ya TDCL ni Mali ya CWT
isipokuwa hayakuwepo makabidhiano rasmi ya usimamizi wa kampuni hiyo.
Aidha amezungumzia kuhusu Benki ya
Mwalimu na kusema kuwa inamilikiwa na walimu kwa asilimia 51.35 na kutoa
mchanganuo wa Umiliki wa hisa.
Bw.Mswanyama amesema kuwa mchanganua
huwa kuwa ni CWT Umiliki hisa 12.94, TDCL hisa 3.23 na Walimu hisa 35.18
ambapo jumla asilimia 51.35 na zingine ni PSPF (PSSSF) 16.17,NHIF
16.17 na Public 16.31 jumla 48.65.
Na pia amezungumzia Mwalimu house na
kusema kuwa ni kitega uchumi cha Chama ambacho kilijengwa kwa kutumia
mapato ya asilimia mbili za wanachama .
No comments:
Post a Comment