Madaktari wakiendelea kuwashauri
wananchi kuhusiana na afya zao katika Hospitali ya Rufaa ya Bugando
jijini Mwanza hivi karibuni.
Wananchi wakiendelea kupewa
utaratibu kuhusiana na matibabu maalum katika wiki ya tiba katika
Hospitali ya Rufaa Bugando jijini Mwanza hivi karibuni.
Dakta Catherine Mung’ong’o Rais wa
Chama Cha Madaktari wa Upasuaji Tanzania akizungumza na Wanahabari
katika Hospitali ya Rufaa Bugando jijini Mwanza hivi karibuni
Madaktari wakiendelea na zoezi la
Opereshi kwa wagonjwa wakati wa siku ya kuhitimisha zoezi la huduma ya
upasuaji kwa wagonjwa wanaosubiri kwa muda mrefu toka Kanda ya Ziwa hivi
karibuni.Zoezi hilo la siku tano limefanyika kwa ushirikiano baina ya
Chama cha Madaktari wa Upasuaji Tanzania na Madaktari wa Hospitali ya
Rufaa ya Bungando. (Na: Mpiga Picha Wetu)
***************************************
Na: Mwandishi Wetu
Zaidi ya wakazi 1000 wa Kanda
ya Ziwa wamenufaika na matibabu bure hasa kwa upande wa upasuaji
unaofanywa na Chama cha Madaktari wa Upasuaji Tanzania.
Hayo yamebainishwa na Rais wa
Chama cha Madaktari wa Upasuaji Tanzania, Dkt. Catherine Mung’ong’o
wakati wa siku ya kuhitimisha zoezi la upasuaji lililofanyika kwa siku
tano kuanzia tarehe 03 hadi 07 Juni 2019 katika Hospitali ya Rufaa ya
Bugando jijini Mwanza.
Alisema kuwa lengo la upasuaji huo
ni kupunguza idadi ya wahitaji wa huduma ya upasuaji kwa wagonjwa
wanaosubiri kwa muda mrefu toka Kanda ya Ziwa, nakuongeza kuwa zoezi
hilo limefanyika kwa ushirikiano baina ya Chama hicho, Madaktari wa
Hospitali ya Rufaa ya Bungando na Madaktari wengine.
Dkt. Mung’ong’o amesema kuwa
huduma hii ya upasuaji inayotolewa na Chama cha Madaktari wa Upasuaji
Tanzania imekuwa ikifanyika kila mwaka katika mikoa mingine huku ni
ikiwa ni mara ya kwanza katika mikoa ya Kanda ya Ziwa.
Kwa upande wake Kiongozi wa Chama
hicho Kanda ya Ziwa ambaye ni Daktari Bingwa wa Upasuaji toka Hospitali
ya Rufaa Bugando, Dkt. Olivia Kimario amesema kuwa zoezi hilo ni
utaratibu uliowekwa na Chama cha Madaktari hao ambapo mwaka huu
wamehudumia katika mikoa ya Mwanza , Shinyanga , Mara na Geita.
Katika hatua nyingine Dkt.
Mung’ong’o amesema kuwa baada ya kukamilisha zoezi hilo la upasuaji kwa
wagonjwa wanaosubiri kwa muda mrefu Chama hicho kitatoa huduma bure za
upasuaji kwa wagonjwa wenye matatizo ya Mdomo Sungura litakalofanyika
tarehe 10 na 11 Juni 2019 bila ya malipo.
No comments:
Post a Comment