Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiagana na viongozi baada ya kufungua
Semina ya Wanahisa wa Benki ya CRDB iliyofanyika kwenye Kituo cha
Mikutano cha Kimataifa cha Arusha (AICC), Mei 17, 2019. Kutoka kushoto ni
Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Benki ya CRDB, Ally Hussein Laay,
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Abdulmajid Musa Nsekela na wa tatu
kushoto ni Balozi wa Denmark chini, Einar Hebogard Jensen. (Picha na Ofisi ya
Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza wakati alipofungua Semina ya
Wanahisa wa Benki ya CRDB kwenye Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Arusha
(AICC), Mei 17, 2019. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa Mei 17, 2019 amefungua Semina
ya Wanahisa wa Benki ya CRDB katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa
cha Arusha (AICC). Pichani, Mheshimiwa Majaliwa akiongozana na
baadhi ya viongozi walioshiriki katika Mkutano huo, kuingia kwenye ukumbi wa
Simba kufungua Semina hiyo. Kutoka kulia ni Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato
Tanzania (TRA), Charles Kicheere, Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Mrisho Gambo,
Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Benki ya CRDB, Ally Hussein Laay
na wa pili kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Abdulmajid Musa
Nsekela. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Autaka uongozi wa benki ya CRDB uzidi
kuzingatia misingi ya utawala bora
WAZIRI MKUU, Kassim Majaliwa ameutaka
uongozi wa Benki ya CRDB uzidikuzingatia misingi ya utawala borana kuongeza
juhudi katika utoaji wa huduma ili benki hiyo iendeleekuwa mfano wa mafanikio
kwa taasisi zinazomilikiwa nakuendeshwa na wazalendo.
Ameyasema hayo leo (Ijumaa, Mei 17,
2019) wakati akifungua semina ya wanahisa wa benki ya CRDB katika Ukumbi wa
Mikutano wa Kimataifa wa Arusha (AICC) jijini Arusha. Semina hiyo inahudhuriwa
na wanahisa 1,500.
Amesema Serikali ya Awamu ya Tano
inayoongozwa na Rais Dkt. John Magufuli imeendelea kuimarisha misingi ya
utawala bora ili kuleta matokeochanya, hivyo ni vema kwa uongozi wa benki hiyo
ukaizingatia.
“Serikali imeendelea kuhakikisha kwamba
katika utekelezaji wa shughuli mbalimbali kunakuwepo na uwazi, uwajibikaji,
ushirikishaji wa watu, ufanisi, tija, uadilifu, usawa, kuzingatia taratibu za
kisheria, kanuni na miongozo inayotolewa na Viongozi wakuu wa kitaifa.”
Waziri Mkuu amesema Serikali
imeendelea kusisitiza misingi hiyo ya utawala bora ili kujiridhisha kuwa
taasisi mbalimbali zikiwemo za kifedha zinaongozwa kwa kufuata misingi
hiyo.
“Serikali imeendelea kusisitiza uwazi
katikakuendesha shughuli za umma na makampuni yanayomilikiwa nawananchi bila
usiri na kificho. Lengo ni kuwapa wananchi uwezo wakupima utendaji na
uzingatiaji wa kanuni, taratibu na sheria.”
Waziri Mkuu amesema lengo la Serikali
ni kuhakikisha wananchi wa jinsia zote na makundi yote wanahusishwa katika
kupanga nakufanya maamuzi ya mambo yanayowahusu ili kuwawezesha kujiletea
maendeleo.
“Nyote ni mashahidi kuwa Serikali
imeendelea kuhimiza utendaji unaozalisha matokeo yanayokidhi lengo
na matarajio ya watu na kuhakikisha taasisi za kifedha zinatimiza ndoto za
wananchi katika kupata huduma nzuri ikiwemo upatikanaji wa mikopo na elimu ya
matumizi bora ya fedha.”
Hivyo, Waziri Mkuu amesema ni vema
benki hiyo kupitia kitengo chake cha elimu ihakikishe inatoa elimu kwa umma juu
ya matumizi mazuri ya fedha zikiwemo za mikopo ili wananchi waweze kuitumia
vizuri na kujiongezea tija.
Awali, Mkurugenzi
Mtendaji wa benki ya CRDB, Abdulmajid Msekela alisema zaidi ya asilimia 80 ya
hisa za benki hiyo zinamilikiwa na Watanzania ikiwemo Serikali, hivyo uongozi
wa benki hiyo una jukumu kubwa la kuhakikisha wanatoa huduma bora.
Alisema wamejipanga kuboresha huduma
zao ili wanahisa waweze kujivunia uwekezaji wao walioufanya kwenye benki hiyo.
“Tupo tayari kuhakikisha benki ya CRDB inasonga mbele zaidi ikiwa ni pamoja na
kuboresha huduma kwa wateja.”
Mkurugenzi huyo alisema kuwa mbali na
kuboresha huduma kwa wateja, pia wataongeza ufanisi katika utoaji wa huduma na
hatimaye waweze kutoa gawio kubwa kwa wanahisa wao. Benki ya CRDB inaongoza kwa
kupata faida kubwa.
Kwa upande wake,Kamishna Mkuu wa
Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Charles Kicheere ambaye alimuwakilisha Waziri
wa Fedha na Mipango katika semina hiyo, alitumia fursa hiyo kuwashauri wananchi
wajenge tabia ya kuwekeza kwenye hisa. Alisema mwamko wa Watanzania
katika kuwekeza kwenye hisa bado ni mdogo.
No comments:
Post a Comment