WAKURUGENZI WA HALMASHAURI WATAKIWA KUSIMAMIA KIKAMILIFU MRADI WA TIMIZA NDOTO ZAKO
Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera,
Uratibu na Uwekezaji) Bi. Dorothy Mwaluko akisisitiza umuhimu wa
Wakurugenzi wa Halmashauri zinazonufaika na mradi wa timiza ndoto
zakoMei 25, 2019 Wilayani Bahi mkoani Dodoma.
Mkuu wa Wilaya ya Bahi Mhe. Mwanahamisi
Mukunda akizungumza wakati wa hafla ya kuzunduliwa kwa mradi wa timiza
ndoto yako Wilayani Bahi mkoani Dodoma.
Mkurugenzi Mtendaji wa Tume ya Taifa ya
Kudhibiti UKIMWI (TACAIDS) Dkt. Leonard Maboko akisisitiza jambo kwa
Katibu mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu na Uwekezaji) Bi Dorothy
Mwaluko ambaye alikuwa mgeni rasmi wakati wa hafla ya kuzindua mradi wa
timiza ndoto zako.
Katibu mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera,
Uratibu na Uwekezaji) akiwa na mkurugenzi wa TAYOA Bw. Peter Masika
mara baada ya kutembelea basi linalotoa huduma za upimaji wa Virusi vya
UKIMWI na UKIMWI wakati wa hafla ya kuzindua mradi wa timiza ndoto zako
Wilayani Bahi mkoani Dodoma.
Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge
ya UKIMWI na Dawa za Kulevya Mhe. Oscar Mukasa akizungumza katika hafla
ya kuzinduliwa kwa mradi huo.
Sehemu ya wanafunzi na wazazi
waliohudhuria hafla ya uzinduzi wa mradi wa timiza ndoto zako
wakifuatilia uzinduzi huo Wilayani Bahi.
Kikundi cha ngoma kikitumbuiza wakati wa hafla ya uzinduzi wa mradi wa timiza ndoto zako.
Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera,
Uratibu na Uwekezaji) Bi Dorothy Mwaluko akiteta jambo na Mkurugenzi
Mtendaji wa Tume ya Kudhibiti UKIMWI Tanzani (TACAIDS) Dkt. Leonard
Maboko wakati wa uzinduzi wa programu hiyo Wilayani Bahi Mkoani Dodoma.
Mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa
la Kupambana na UKIMWI (UNAIDS) Bw. Koech Rotich katika hafla ya
kuzindua mradi wa Timiza ndoto yako Bw. Akizungumza wakati wa uzinduzi
wa huo Wilayani Bahi.
Sehemu ya wanufaika wa mradi wa Timiza
ndoto zako wakitoa shuhuda za mafunufaa wanayopata kupitia mradi huo na
kupongeza Serikali kwa kuwezesha utekelezaji wa mradi huo
Baadhi ya wazazi wa wanafunzi wanaonufaika na mradi wa timiza ndoto zako wakitoa ushuhuda wa faida za mradi huo .
Mbunge wa Bahi Mhe.Omary Baduel
akisisitiza umuhimu wa wanufaika wa mradi wa timiza ndoto zako kutumia
mradi huo kujikwamua na kujiletea maendeleo.
(Picha zote na Ofisi ya Waziri Mkuu)
………………..
Na Mwandishi Wetu
Wakurugenzi 10 wa Halmashauri za Wilaya
wametakiwa Kuhakikisha kuwa mradi wa timiza ndoto zako kwa wasichana
Balehe waliopo mashuleni na walio nje ya mfumo wa elimu unatekelezwa
kama ilivyopangwa na Serikali ili kuleta matokeo chanya.
Akizungumza kwa niaba ya Waziri wa Nchi,
Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu
Mhe. Jenista Mhagama Mei 25, 2019 Wilayani Bahi mkoani Dodoma wakati wa
uzinduzi wa mradi huo, Katibu Mkuu Ofisi hiyo anayeshughulikia Sera
Uratibu na Uwekezaji Bi. Dorothy Mwaluko amesema kuwa dhamira ya
Serikali ni kuona mradi huo unaleta ukombozi wa kweli kwa mtoto wa kike.
“ Waliopo shuleni na nje ya mfumo wa
elimu ni vyema mkatambua kuwa mradi huu ni fursa yakuwawezesha
kujikwamua kiuchumi na kuepeuka vishawishi na maambukizi ya Virusi vya
ukimwi kwani Serikali inatambua kuwa kumuwezesha mtoto wa kike ni
kuiwezesha jamii nzima”Alisema Bi. Doorthy.
Mradi huu unatekelezwa katika mikoa ya
Dodoma, Morogoro na Singida ambapo jumla ya Halmashuri 10 katika mikoa
hiyo zinanufaika.Utekelezaji wake unatokana na usaidizi wa fedha kutoka
kutoka Mfuko wa Dunia kwa ajili ya kuendeleza mapambano dhidi ya
maambukizi ya Virusi vya UKIMWI na athari zake.
Akifafanua amesema kuwa watekelezaji wa
mradi huo wanalo jukumu la kuwajengea uwezo wanaufaika ili hata baada ya
kipindi cha mradi waweze kujitegemea na kuondokana na utegemezi kutoka
kwa serikali ambapo kwa sasa wanafunzi kutoka Kaya masikini wanawezeshwa
kupata taulo za kujisitiri pamoja na mahitaji mengine ikiwemo sare za
shule.
Aliongeza kuwa wanafunzi wote wanapaswa
kutambua kuwa Serikali inawekeza fedha nyingi katika mradi huo kwa
kutambua umuhimu wa kundi hilo ili kujikwamua kielimu na kutumia vyema
vipaji walivyo navyo.
Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Bahi
Mhe. Mwanamisi Mukunda akizungumza kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa huo Dkt.
Binilith Mahenge amasema kuwa mradi huo umesaidia kuongeza kiwango cha
ufaulu katika Wilaya hiyo, mahudhurio ya wanafunzi shuleni yameongezeka
kwa kiwango kikubwa.
“Tunaishukuru Serikali ya Awamu ya Tano
kwa kutuletea mradi huu katika Wilaya yetu kwani umeonesha mafanikio
makubwa kwa kipindi cha majaribio ambacho umetekelezwa kwani
umewanufaisha Wanawake Vijana wenye umri wa kati ya miaka 10- 24”,
alisisitiza Mhe. Mwanahamisi.
Akifafanua amesema kuwa mradi huo
umefikia Kaya 265 na wasichana 129 unawanufaisha wasichana balehe
waliopo shuleni na wale wa nje ya shule 45.
Naye Mkurugenzi Mtendaji wa Tume ya Taifa
ya Kudhibiti Ukimwi (TACAIDS) Dkt. Leonard Maboko amesema kuwa mradi
huo ni wa miaka 3 na unatekelezwa katika mikoa 3 ambapo wanufaika wa
mradi walio nje ya shule watajengwewa uwezo kwa kupewa stadi za maisha.
Alitaja sababu za kuwalenga wasichana
wanaobalehe Dkt. Maboko amesema kuwa ni pamoja na kundi hilo hilo kuwa
waathirika wakubwa ambapo asilimia 80 ya maambukizi ya VVU yamewaathiri
vijana wa kundi hilo.
Mmoja wa wazazi wa wanafunzi walionufaika
na mradi huo Bi Mayasa Mussa amesema kuwa wanafunzi wanafurahia mradi
huo na ari ya kwenda shule imeongezeka kwani kila mwezi wanapokea elfu
25,000/- kwa mwezi kuwawezesha kukidhi mahitaji muhimu ya wanafunzi hao
ikiwemo kupata taulo za kike, sare za shule na mahitaji mengine.
Mradi wa Timiza ndoto zako unatekelezwa
katika mikoa 3 na Halmashuri na Halmashuri 10 ukilenga kuwawezesha
wasichana waliobalehe wakiwa mashuleni na wale walio nje ya mfumo wa
elimu.
No comments:
Post a Comment