WAZIRI NDALICHAKO AIPA KAZI NACTE
Waziri wa Elimu Sayansi na Technolojia
Prof.Joyce Ndalichako akipokea maelekezo kutoka kwa Mhadhiri wa Chuo
Mipango Ezekiel Kanire, juu ya kazi mbalimbali zinazofanywa na Chuo
hicho wakati wa maonyesho ya kwanza ya Elimu na mafunzo jijini Dodoma.
Waziri
wa Elimu Sayansi na Technolojia Prof.Joyce Ndalichako akipokea
maelekezo kutoka kwa Mhadhiri wa Chuo Mipango Ezekiel Kanire, juu ya
kazi mbalimbali zinazofanywa na Chuo hicho wakati wa maonyesho ya kwanza
ya Elimu na mafunzo jijini Dodoma.
Waziri wa Elimu Sayansi na Technologia
Prof.Joyce Ndalichako akipokea maelekezo kutoka kwa Mkufunzi wa chuo cha
Dare es saalam institute Technology juu ya kazi zinazofanyika chuoni
hapo wakati wa maonyesho ya mabanda ya vyuo vya kati jijini Dodoma.
Askari wa kikosi cha zima moto na uokoaji
akionyesha namna ya kuzima moto, wakati wa ufunguzi wa wiki ya
maonyesho ya kwanza ya Elimu ya ufundi na mafunzo ya nayofanyika Jijini
Dodoma.
Msajili wa chuo cha Bandari cha Dar es
Saalam wa kwanza kushoto, Jonneo Lugoye akitoa maelezo kwa Waziri wa
Elimu Sayansi na Technolojia Prof, Joyce Ndalichako juu ya kazi
zinazofanywa na chuo hicho, wakati wa maonyesho kwanza ya Elimu ya
Ufundi na Mafunzo yanayofanyika Jijini Dodoma.
Waziri wa Elimu Sayansi na Technolojia,
Prof, Joyce Ndalichako katikati akiselebuka pamoja na msanii maarufu
Mrisho Mpoto kushoto, kulia ni Mkuu wa Wilaya ya Dodoma Patrobus Katambi
wakati wa ufunguzi wa wiki ya maonyesho ya kwanza ya Baraza la Elimu
ya Ufundi na Mafunzo Jijini Dodoma.
Katibu Mtendaji wa Baraza la Elimu ya
Ufundi na Mafunzo Tanzania Adolph Rutayuga, akizungumza wakati wa
ufunguzi wa wiki ya Maonyesho Elimu ya Ufundi na Mafunzo yanayofanyika
Jijini Dodoma.
Mkuu wa Wilaya ya Dodoma Patrobus Katambi
akizungumza wakati wa ufunguzi wa wiki ya Maonyesho Elimu ya Ufundi na
Mafunzo yanayofanyika Jijini Dodoma.
Makamu mwenyekiti wa Kamati ya huduma za
kijamii, ambaye ni Mbunge wa jimbo la Chemba, Mh, Juma Nkamia
akizungumza wakati wa ufunguzi wa wiki ya Maonyesho Elimu ya Ufundi na
Mafunzo yanayofanyika Jijini Dodoma.
Mwenyekiti wa Baraza la Elimu ya Ufundi
na Mafunzo Bw, John Kondoro akizungumza wakati wa ufunguzi wa wiki ya
Maonyesho Elimu ya Ufundi na Mafunzo yanayofanyika Jijini Dodoma.
Waziri wa Elimu Sayansi na Technolojia
Pro, Joyce Ndalichako akihutubia mamia ya washiriki wa ufunguzi wiki ya
maonyesho ya Elimu ya Ufundi na Mafunzo yanayofanyika Jijini Dodoma.
Waziri wa Elimu Sayansi na Technolojia
Prof, Joyce Ndalichako akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya
washiriki wakati ya ufunguzi wa wiki ya Elimu ya Ufundi na Mafunzo
yanayofanyika Jijini Dodoma.
Picha na Alex Mathias -Wazo-huru blog
………………….
Na.Alex Mathias,Dodoma
WAZIRI wa Elimu Sayansi na Technolojia
Prof. Joyce Ndalichako amelitaka baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi
Tanzania, NACTE, kujenga utamaduni wa kuvitembelea mara kwa mara vyuo
vilivyo chini ya baraza hilo ili kuhakikisha elimu inayotolewa na vyuo
hivyo iwe ya kiwango, ili kufikia malengo ya Serikali.
Prof. Ndalichako ameyasema hayo leo
Jijini Dodoma wakati akifungua maonyesho ya kwanza ya Elimu ya Ufundi na
Mafunzo, yaliyoandaliwa na baraza hilo yenye lengo la kuvikutanisha
vyuo vilivyochini ya balaza hilo.
Amesema ni lazima NACTE ijenge utamaduni
wa kuvitembelea vyuo hivyo ili viweze kutoa mafunzo bora yatakayo
saidia katika mkakati wa Serikali na kufikia malengo ya ujenzi wa
Tanzania ya viwanda.
Amesema kama vyuo hivyo hazitatoa elimu
na mafunzo bora lengo la kufikia nchi ya viwanda halitafanikiwa, ni
wajibu wa baraza hilo kuhakikisha inasimamia utoaji wa mafunzo yaliyo
bora.
“Pia niwatake ninyi baraza kama walezi wa
hivi vyuo hebu mjenge utamaduni na tabia ya kuvitembelea vyuo hivyo
vilivyochini yenu angalau vitoe elimu bora, kataka kufikia malengo ya
serikali kufikia nchi ya viwanda, na tutafikia kwa kuhakikisha vyuo hizi
vinatoa mafunzo bora” amesema Prof. Ndalichako.
Pia amesema serikali haitasita kukifungia
chuo chochote kitakachokutwa kinaendeshwa kinyume na ithibati
iliyotolewa na serikali, kwani itakuwa ni kinyume na taratibu
zilizowekwa na serikali.
Pia amevitaka vyuo hivyo kutumia
maonyesho kubadilishana mawazo, na namna ya kutoa mafunzo bora na kukuza
ushirikiano baina ya taasisi, wadau wa maendeleo pamoja na waajiri
mbalimbali katika kuuza sekta hiyo.
Amesema katika kuhakikisha elimu hiyo
inakuwa serikali kupitia wizara hiyo imetenga kiasi cha milioni kumi na
nane(18,000,000) kujenga chuo kikubwa cha ufundi jijini Dodoma
kitakachosaidia kukuza elimu ya ufindi, pia imetengwa bilion arobaini
kujenga vyuo vingine ishirini na tano (25) maeneo mbalimbali.
Sambamba na hilo serikali imepanga
kukarabati vyuo hamsini na nne(54) vya ufundi ili kufikia kutoa mafunzo
yaliyobora, na kuongeza udahili wa wanafunzi wa ufundi mbalimbali hapa
nchini.
Kwa upande wake katibu mtendaji wa NACTE
Adolph Rutayuga amesema tangu kuanzishwa kwa baraza hilo mwaka 1997 na
kuanza rasmi kazi zake mwaka 2001 wamefanikiwa kudhibiti uanzishwaji wa
vyuo vya ufundi kiholela.
Amesema jumla ya vyuo vyote ni mia tano
arobaini(540) na kati ya hivyo mia mbili hamsini na moja ni vya umma na
mia tatu kumi na tisa na vya binafsi na kati ya hivyo vyuo ishirini na
moja havikukidhi matakwa na vilifutwa kabisa usajiri wake.
Maonyesho hayo yatakayo dumu kwa siku
tano yanayofanyika katika uwanja wa Jamhuri Dodoma, umebebwa na kauli
mbiu isemayo “Elimu ya ufundi na mafunzo kwa maendeleo ya uchumi wa
viwanda Tanzania”
No comments:
Post a Comment