Thursday, May 16, 2019

Wafanyabiashara Jijini Dodoma Waunga Mkono Katazo la Matumizi ya Mifuko ya Plastiki


Na: Mwandishi Wetu, Dodoma
Baadhi ya wafanyabiasha katika Jiji la Dodoma wametoa maoni yao kuhusu katazo la matumizi na biashara ya mifuko ya plastiki ifikapo tarehe 1 Juni 2019 nakusema kuwa katazo hilo limekuja wakati sahihi.
Akizungumza na mwandishi wetu Katibu Mkuu wa Soko Kuu la Majengo, Jijini Dodoma, Eliamani Mollel amesema kuwa wao kama viongozi wamepokea na kuunga mkono marufuku ya kutotumia na kufanya biashara ya mifuko ya plastiki, Serikali ina nia ya dhati kabisa kukataza hii mifuko kutokana na uharibifu wa mazingira, sisi wenyewe ni mashuhuda tunaona mifuko inaleta uharibifu wa mazingira, kuziba kwa mitaro ya maji na adha zingine nyingi zinazofanana na hizo, kwa hiyo sisi kama viongozi kwa kushirikiana na Afisa Mtendaji , jiji kwa ujumla tunaunga mkono hili la Wazari Mkuu la kukataza matumizi ya mifuko ya plastiki.
Akichangia maoni hayo Mfanyabiashara wa Vifungashio vya biadhaa ikiwemo mifuko ya plastiki katika Soko la Majengo Jijini Dodoma, Isack amesema kuwa licha ya mud uliotolewa kuwa mfinyu lakini yupo tayari kuhakikisha ifikapo tarehe 1 Juni 2019 anakuwa amekwisha acha kuuza mifuko ya plastiki baadala yake atakuwa anauza mifuku ambayo inakubalika kwa mujibu wa katazo hilo lililotolewa na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa hivi karibuni.
Naye Evarist Korneli Sanzi, Mfanyabiashara wa Soko la Changombe Jijini Dodoma amesema kuwa binafsi amefurahishwa sana na katazo la matumizi ya mifuko ya plastiki lililotolewa na Waziri Mkuu kwani mifuko hiyo imekuwa ikiharibu mazingiora na uchafu na kuongeza kuwa kama angekuwa na uwezo angekuwa amekemea siku nyingi sana kwa sababu imekuwa ni kero, lakini aliposikia tamko la Waziri Mkuu amefurahi sana.
Mfanyabiashara mwingine aliyechangia maoni yake, Badiliko Ally Ndudi, ambaye ni mfanyabiashara wa vifungashio katika Soko la Majengo jijini Dodoma amesema kuwa pamoja na changamoto zitakazojitokeza lakini katazo la matumizi ya plastiki amesema kuwa mifuko ya plastiki ina athari kwa afya ya binadamu kwa mujibu wa wanasayansi walivyodai.
Mfanyabiashara wa Soko Kuu la Majengo Jijini Dodoma, Urban Munishi anasema kuwa katazo la matumizi ya mifuko ya plastiki  kwake ni fursa kutokana na aina ya bidhaa anayouza ikiwa ni nafaka pamoja na vikapu. Anasema kuwa wateja wa vikapu wameongezeka na mifuko ya sandarusi wameongezeka mara baada ya tangazo la marufuku ya matumizi ya mifuko ya plastiki ifikapo Juni Mosi 2019.
Kwa upande wake mnunuzi wa bidhaa katika Soko la Majengo jijini Dodoma, Bi. Josinah Leornad amesema kuwa amefurahishwa sana na katazo hili la matumizi ya mifuko ya plastiki kwani imekuwa kero kwani ulikuwa kila ukinunua kitu kidogo unafungiwa kwenye mifuko hiyo unajikuta nyumbani unakuwa na mifuko mingi sana na baadae ukiichoma moshi wake ni hatari kwa afya kwa hiyo nimefurahi kusikia wanaleta mifuko mbadala ambayo pia itakuwa rafiki kwa mazingira kwasabubu mifuko ya plastiki imekuwa ikisababisha vyanzo vya maji kuharibika, mitaro kuziba hivyo kusitishwa kwake kuta okoa mazingira.
Mwenyekiti wa Soko la Chang’ombe jijini Dodoma anasema kuwa katazo la matumizi ya mifuko ya plastiki wanaliunga mkono kwani kwao ni kama limepiga ndege wawili kwa jiwe moja kwanza kulinda mazingira ambayo mifuko imekuwa ikizagaa zagaa lakini pili linawapa ahueni wafanyabiasha kwakuwa wamekuwa wakipata hasara kutokana na kugawa mifuko bure kwa wateja wao.
Amesema kuwa vifungashio mbadala ni rafiki kwa mazingira kutokana na malighafi iliyotumika kutengenezea mifuko hiyo, ameipongeza Serikali kwa uhamasishaji mkubwa ilioufanya hasa kwa kuhakikisha wananchi wote wanapata ujumbe mfupi wa kwa njia ya simu kuhusu katazo hilo hivyo anaimani kuwa ifikapo tarehe 1 Juni 2019 hakuna mwananchi atakayekuwa anatumia mifuko ya plastiki labda awe ameau kukaidi kwa makusudi tu.
Hassan Ramadhan Kikoro, mfanyabiashara wa nafaka na vifungashio Soko la Chang’ombe Jijini Dodoma amesema kuwa kutokana katazo hili la matumizi ya mifuko ya plastiki ameanza kuuza mifuko mbadala ambapo amesema kuwa ifikapo tarehe 31 Juni 2019 kama bado atakuwa na bidhaa ya mifuko ya plastiki ataichoma moto ili kuendana na amri iliyotolewa na Serikali, na kuongeza kuwa anafahamu athari zitokanazo na mifuko ya plastiki ila wamekuwa wakiiuza kwakuwa hakukuwa na mifuko mbadala wala katazo lolote.
Kwa upande wake mfanyabiashara wa Soko la Chang’ombe, Bibi. Elizabeth Boniphace Risasi ameishukuru Serikali kwa kupiga marufuku matumizi ya mifuko ya plastiki kwa kuwa kwake binafsi imemcheleweshea maendeleo kwakuwa bidhaa zake anazouza (vikapu) kutonunuliwa kutokana na uwepo wa mifuko hiyo licha ya ukweli kwamba inachangia kwa kiasi kikubwa uharibifu wa mazingira.
Mwisho

No comments:

Post a Comment