LAZARO NYALANDU MIKONONI MWA TAKUKURU , ASHIKILIWA KWA MAHOJIANO
TAASISI ya Kuzuia na Kupambana na
Rushwa (TAKUKURU) inamshikilia aliyewahi kuwa Waziri wa Maliasili na
Utalii Lazaro Nyalandu kwa tuhuma za vitendo vinavyoashiria uwepo wa
rushwa.
Nyalandu ambaye kwa sasa ni Kada wa
Chadema amekamatwa leo saa tisa Alasiri mkoani Singida ambapo baada ya
kukamatwa amechukuliwa na kwenda kuhojiwa na TAKUKURU.
Akiongea kwa njia ya simu jioni
hii, Mkuu wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa(TAKUKURU)Mkoa wa
Singida Joshua Msuya amesema Nyalandu wamemkamata leo kutokana na
kufanya vitendo vinavyoashiria uwepo wa rushwa.
“Ni kweli tumemkamata Nyalandu kwa
ajili ya kufanya naye mahojiano, kuna mikutano ya kisiasa ambayo
wanaifanya na kuna viashiria vya vitendo vya rushwa.Hivyo tumemkamata
kwa ajili ya kumhoji.Tunaomba ifahamike tunamhoji kwasababu ya kuwepo
viashiria vya vitendo vya rushwa na si kwamba tumemkamata akitoa
rushwa,”amesema Msuya.
Alipoulizwa kama bado wanamshikilia
au laa ,Msuya amejibu wao baada ya kumhoji wamemkabidhi kwa vyombo
vingine vya ulinzi na usalama kwa mahojiano zaidi.
Taarifa za kwamba amevamiwa na watu
wasiojulikana wakia na silaha, Joshua amejibu sio kweli kwani Nyalandu
kabla ya kuchukuliwa kwa ajili ya kuhojiwa alipewa taarifa na hivyo
alikuwa anajua kuwa anahitajika TAKUKURU.
No comments:
Post a Comment