Wednesday, February 20, 2019

ZIARA YA MAKAMU WA RAIS WILAYANI MKALAMA

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza na wananchi wa kijiji cha Ibaga wilaya ya Mkalama ambao waliusimamisha msafara wake kwa lengo la kumsalimu ,Makamu wa Rais yupo kwenye ziara ya kikazi mkoani Singida. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akipata maelezo ya maendeleo ya ujenzi wa daraja la Sibiti kutoka kwa Kaimu Meneja Wakala wa Barabara Tanzania (TANROADS) mkoa wa Singida Mhandisi Matari J. Masige (kushoto) ambalo limekamilika kwa asilimia 94.8%,kulia ni Mkuu wa mkoa wa Singida Dkt. Rehema Nchimbi. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)
 Muonekano wa daraja la Sibiti ambalo kwa mujibu wa taarifa za Wakala wa Barabara Tanzania (TANROADS) walizozitoa wakati wa ziara ya Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassa ambapo wamesema ujenzi wake umekamilika kwa asilimia 94.8%. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akipata maelezo ya maendeleo ya ujenzi wa daraja la Sibiti kutoka kwa Kaimu Meneja Wakala wa Barabara Tanzania (TANROADS) mkoa wa Singida Mhandisi Matari J. Masige (kushoto) ambalo limekamilika kwa asilimia 94.8%,kulia ni Mkuu wa mkoa wa Singida Dkt. Rehema Nchimbi. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano Mhe. Samia Suluhu Hassan leo ameenndelea na ziara yake ya kukagua na kuhamasisha shughuli za kimaendeleo mkoani Singida ikiwa ni siku ya nne ya ziara mkoani humo.

Akizungumza na wananchi waliojitokeza kwenye eneo la mradi wa ujenzi wa Daraja Sibiti, Makamu wa Rais amesema huu ni wakati muafaka  kwa kila Mtanzania kufanya kazi kwa bidi ili kuleta maendeleo nchini.

“Tufanye kazi kwa bidii ili tuweze kuleta maendeleo yetu, miradi yote mnayoiona mikubwa inajengwa 80% ni kwa fedha za ndani”alisema Makamu wa Rais.

Makamu wa Rais amewataka Watanzania kwa ujumla kuwa walinzi wa miundombinu mbali mbali inayojengwa na Serikali.

“Miundombinu hii ni ya kwenu wala si ya Serikali hivyo kila mwananchi ana wajibu wa kuwa mlinzi na kutoa taarifa kwa vyombo vya usalama pindi wanapoona uharibifu unafanyika”alisisitiza Makamu wa Rais.

Aidha aliwaambia wananchi hao kuwa Serikali ya Awamu ya Tano imedhamiria kuhakikisha kila mwananchi anapata huduma bora ya afya na kwa sasa inakuja na mpango wa bima kwa wote ambao kila mwananchi atalazimika kuwa na bima hiyo.


Ujenzi wa Daraja la Sibiti unaogharimu zaidi ya bilioni 16 umefikia asilimia 94.8%, daraja hili lina urefu wa 82 na upana wa mita 7.1ni kiungo muhimu kati ya mkoa wa Singida na Simiyu pamoja mikoa ya Arusha na Manyara.


Kwa upande mwingine Naibu Waziri Ujenzi Mhe. Elias Kwandikwa amesema Serikali inatekeleza miradi mikubwa 19 ya ujenzi wa madaraja makubwa nchi nzima.

Wakati huohuo Waziri wa Madini Mhe. Doto Biteko amesema kuwa daraja la Sibiti litasaidia sana kusafirishia chumvi pamoja na madini ya kopa.

Nae Naibu Wizara ya Maji Mhe. Juma Aweso amesema kuwa katika wilaya ya Mkalama zaidi ya bilioni 2 zimetumika kutekeleza miradi ya maji na visima 18 virefu vimechimbwa wilayani humo.

 Pamoja na mambo mengine Makamu wa Rais alitembelea shule ya Sekondari ya Iguguno ambayo ilipatiwa zaidi ya shilingi milioni 400 kwa ajili ya kukarabati na kujenga miundombinu ya kidato cha tano na chasita, bweni na bwalo, na kuweka jiwe la msingi la uzinduzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Mkalama.

No comments:

Post a Comment