Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akimkabidhi Diwani wa Kata ya Muhange
wilayani Kakonko, Ibrahim Katunzi jumla ya shilingi milioni moja kwa ajili ya
Mradi wa Maji na Zahanati katika Kata hiyo, Februari 19, 2019.
(Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiwapungia wananchi wakati alipowasili
kwenye eneo la Mradi wa Maji wa Muhange wilayani Kakonko kukagua
mradi huo, Februari 19, 2019. Kulia ni mkewe Mary na kushoto ni Mbunge wa
Buyungu, Mhandishi Christopher Chiza. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Mke wa Waziri Mkuu, Mama Mary Majaliwa akiwasalimia
wananchi wa kijiji cha Muhange wilayani Kakonko wakati Waziri Mkuu,
Kassim Majaliwa alipokagua Mradi wa Maji kijijini hapo, Februari 19, 2019.
(Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na wananchi baada ya
kakagua Mradi wa Maji wa Muhange wilayani Kakonko, Februari 19,
2019. Wengine kutoka kushoto ni Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya
Nchi, Mhandisi Hamadi Masauni, Mkuu wa Mkoa wa Kigoma, Brigedia Jenerali
Mstaafu, Emmanuel Maganga, Mbunge wa Buyungu Mhandisi Christopher Chiza, Mke wa
Waziri Mkuu, Mama Mary Majaliwa, Waziri wa Elimu, Sayansi na Tekinolojia,
Profesa Joyce Ndalichako na kulia ni Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara,
Mhandisi Stella Manyanya. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
No comments:
Post a Comment