Katibu Tawala Mkoa wa Songwe David Kafulila akizungumza na watumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya Ileje ambapo amewasisitiza kutimiza majuku yao na kutii sheria na kanuni za utumishi wa umma.
Katibu Tawala Mkoa wa Songwe David Kafulila akitembea kukagua kaya zinazonufaika na Mpango wa TASAF katika Kijiji cha Ilulu Wilayani Ileje ili kujionea utekelezaji wa mpango huo.
Katibu Tawala Mkoa wa Songwe David Kafulila akikagua baadhi ya nyaraka katika Ofisi ya Mtendaji wa Kijiji cha Ilulu Wilayani Ileje wakati akikagua utekelezaji Mpango wa TASAF katika Kijiji hicho.
xxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxx
Katibu Tawala Mkoa wa Songwe David Kafulila amefanya ziara Wilayani Ileje ambapo ameanza kwa kuzungumza na watumishi wa Halmashauri hiyo, amekagua Ujenzi wa Hospitali ya Wilaya ya Ileje na kutembelea kaya za Wanufaika wa Mpango wa TASAF ambapo haya ndiyo yaliyojiri;
i. Katibu Tawala Mkoa wa Songwe David Kafulila amekuja kuwakumbusha sheria, kanuni na taratibu za Utumishi wa Umma kwakuwa yeye ndiye Mkuu wa Utumishi wa Umma Mkoa wa Songwe- Katibu Tawala Msaidizi Utawala na Utumishi, Chele Ndaki
ii. Napenda kuwakumbusha watumishi wote kuheshimu mamlaka zilizopo Kisheria na kuzingatia sheria zote za utumishi wa umma - Katibu Tawala Msaidizi Utawala na Utumishi, Chele Ndaki
iii. Watumishi hakikisheni kuwa mnatimiza majukumu yenu wakati mnadai maslahi yenu yaani kama kuna mambo mnadai sio sababu ya kuweka uzembe katika utumishi wenu- Katibu Tawala Mkoa wa Songwe David Kafulila
iv. Tulisaini Mkataba wa utumishi kwenye sekta za elimu na afya kwa kuwekeana vigezo ambavyo vitapimwa mwezi huu wa pili na mwezi wa tatu tutafanya tathmini, wale watakao shindwa kufikia vigezo hivyo tutawaondoa ili wawekwe wengine ambao watafanya vizuri - Katibu Tawala Mkoa wa Songwe David Kafulila
v. Kwa mujibu wa sheria za utumishi zinaruhusu mtumishi aliyeshindwa kutimiza wajibu wake kufukuzwa kazi au kunyang’anywa cheo, sio mpaka uibe - Katibu Tawala Mkoa wa Songwe David Kafulila
vi. Kama taasisi wote tunatakiwa kuongeza ufanisi wa uendeshaji wa kazi zetu, kama Mkoa tumeanzisha mfumo wa kupima utendaji wa watumishi unaoitwa Songwe Task Information Management System, kwa mfumo huu tutakuwa wa kwanza kuutumia nchini na utawezesha kufahamu utendaji wa kila siku wa watumishi wote- Katibu Tawala Mkoa wa Songwe David Kafulila
vii. Mtendaji yeyote atakaye shindwa kutekeleza agizo la Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. John Pombe Magufuli la kuhakikisha kila mjasiriamali mdogo anapatiwa kitambulisho, hususani kwa kipindi kilichobaki cha wiki tatu, hilo ni kosa ambalo linatosha kumfukuzisha kazi- Katibu Tawala Mkoa wa Songwe David Kafulila
viii. Ujenzi katika Hospitali ya Wilaya ya Ileje Umesitishwa mpaka hapo kasoro zilizooneka zirekebishwe, awali ili ripotiwa kuwa kwenye beam kuna ufa na kusababisha mpasuko kwa ndani na Kupinda lakini tumekagua na kubaini sehemu ya juu imetitia kwa ndani, hili ni tatizo kubwa kuliko lilivyo ripotiwa awali- Katibu Tawala Mkoa wa Songwe David Kafulila
ix. Mkurugenzi wa Halmashauri ya Ileje ahakikishe waliohusika wote na ujenzi mbovu katika Hospitali ya Ileje popote pale walipo watafutwe na wachukuliwe hatua kali lakini pia Mkurugenzi ahakikishe ifikapo Juni 30, 2019 fedha zilizoletwa na serikali shilingi Bilioni 1.5 ziwe zimetumika kuendeleza ujenzi wa hospitali hiyo baada ya kurekebisha maeneo hayo yenye dosari -Katibu Tawala Mkoa wa Songwe David Kafulila
x. Kuna umuhimu mkubwa wa kurekebisha makossa hayo yaliyojitokeza na kuendeleza ujenzi bila kufanya hivyo kunaweza kusababisha maafa yaani jengo hili kuanguka, Makosa yaliyofanyika ni ya design ndio maana eneo lililotitia limesababishwa na uzito wake wenyewe hivyo huwezi kuendelea na ujenzi wa ghorofa hili la hospitali- Meneja wa TARURA Wilaya ya Ileje Mhandisi Lugano Mwambingu
xi. Tunakiri hatukuona matatizo hayo mapema ila nia yetu ni kuhakikisha marekebisho hayo yanatekelezwa, jambo hili limetuathiri kwani nasi tulitarajia ghorofa hili likamilike ili wananchi wetu wanufaike na huduma katika hospitali hii- Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Ileje Joseph Mchome
xii. Katika ziara hii pia nimebaini kuwa Kuna tatizo la serikali la vijiji kuendeshwa kwa kutofuata taratibu hasa kutofanya mikutano ya vijiji na kutotunza kumbumbuku za vijiji licha ya kuwa serikali imeajiri watendaji wenye diploma - Katibu Tawala Mkoa wa Songwe David Kafulila
xiii. Nawaagiza wakurugenzi wote Mkoa wa Songwe wafuatilie utendaji wa serikali ngazi ya vijiji, ili mapato na matumizi yabandikwe, vikao vya kisheria vifanyike na kuwepo file la mihtasari ya vikao vyote vya kijiji kwakuwa haya ni matakwa ya kisheria - Katibu Tawala Mkoa wa Songwe David Kafulila
xiv. Wajibu wa Halmashauri na waratibu wa TASAF ni kuhakikisha fedha zinawafikia walengwa na hakuna kaya hewa aidha wakaguzi wa ndani wakague fedha za TASAF kama mfuko maalumu tofauti na sasa wanavyofanya ukaguzi wa jumla ukizingatia hizi ni fedha nyingi kwani serikali kwa mkoa wa Songwe ni imetoa zaidi ya bilioni 14 kwa mpango huo- Katibu Tawala Mkoa wa Songwe David Kafulila
xv. Halmashauri itaendelea kusimamia watendaji wa vijiji na kata ili watimize majukumu yao kisheria, tumekuwa tukiwachukulia hatua watendaji ambao hawatimizi majukumu yao na tutaendelea kufanya hivyo - Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Ileje Joseph Mchome
xvi. Tunashukuru mpango wa TASAF kwakuwa umetukomboa kimaisha, ijapokuwa mimi ni mjane nimeweza kupata mbolea na chakula kupitia fedha za TASAF, hivyo nawashukuru sana walio anzisha mpango huu-Hana Mtawa Mkaji wa Kijiji cha Ilulu, Ileje na Mnufaika wa TASAF
No comments:
Post a Comment