Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akihutubia
wasanii wa fani mbali mbali waliohudhuria Kongamano Kuhusu Tatizo la Dawa
za Kulevya kwa Wasanii lililoandaliwa na Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na
Dawa za Kulevya pamoja na Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo leo
februari 13, 2019 lililofanyika katika Kituo cha Kimataifa cha
Mwalimu Julius Nyerere, jijini Dar es Salaam. (Picha na Ofisi ya Makamu wa
Rais)
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiangalia
kwa umakini Sanaa ya maigizo iliyokuwa ikionyeshwa na wasanii kutoka Taasisi ya
Sanaa na Utamaduni Bagamoyo (TASUBA) waliokuwa wakionyesha madhara ya dawa ya
kulevya wakati wa Kongamano Kuhusu Tatizo la Dawa za Kulevya kwa Wasanii
lililoandaliwa na Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya pamoja
na Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo leo februari 13, 2019
.Kongamano hilo limefanyika katika Kituo cha Kimataifa cha Mwalimu
Julius Nyerere, jijini Dar es Salaam. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)
Heshima kwa Godzilla; Wasanii wa Filamu na Muziki wakiwa wamesimama kwa dakika
moja kama ishara ya kumkumbuka msanii wa hiphop Tanzania Golden Jacob
Mbunda aliyefariki asubuhi ya leo kabla ya kuanza kuhutubia Kongamano
Kuhusu Tatizo la Dawa za Kulevya kwa Wasanii lililoandaliwa na Mamlaka ya
Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya pamoja na Wizara ya Habari,
Utamaduni, Sanaa na Michezo leo februari 13, 2019
lililofanyika katika Kituo cha Kimataifa cha Mwalimu Julius
Nyerere, jijini Dar es Salaam. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu
Hassan amewataka wasanii chini kuiga mambo yenye kuleta manufaa kwa jamii.
Makamu wa Rais ameyasema hayo leo jijini Dar es Salaam wakati akihutubia
Wasanii wa Sanaa mbalimbali waliohudhuria Kongamano la Wasanii nchini dhidi ya
tatizo la dawa za kulevya.
“Naamini kuwa wasanii hawa ni vioo vya jamii lakini
baadhi yao wamekuwa wakitumika kama ‘mapunda’ kusafirisha dawa na wengine
kudumbukia kwenye uraibu wa dawa za kulevya” alisema Makamu wa Rais.
Makamu wa Rais aliwaasa wasanii hao kujiepusha na matumizi na biashara
ya dawa za kulevya ambapo aliwaambia dawa za kulevya zina madhara mengi
kiuchumi, kisiasa, mazingira, kiafya na kijamii, pia hudhoofisha afya za
watumiaji na kuathiri uwezo wa kufanya kazi.
Kongamano hilo lililobeba kauli mbiu inayosema Usanii bila
kutumia au kubeba Dawa za Kulevya inawezekana, Chukua Hatua.
Makamu wa Rais amepongeza kwa kuanzisha vituo 6 vya huduma ya methadone
ambapo jumla ya waathirika 6,300 wametibiwa kwenye vituo hivi.
Makamu wa Rais ameagiza Mamlaka ya Chakula na Dawa (TFDA)
kuharakisha miongozo hiyo na itakuwa vyema ikiwa kwenye udhibiti wa
Dawa za hospitali zenye asili ya kulevya ili zitolewe na Bohari ya Kuu ya
Madawa (MSD) badala ya watu binafsi.
Pamoja na mambo mengine Makamu wa Rais ametoa rai kwa vyombo vya ulinzi
na usalama hususani polisi na maafisa uhamiaji kuhakikisha kuwa bidhaa
zinazovuka mipaka yetu zisiwe bidhaa zinazokuja kuharibu Taifa.
Kwa upande mwingine Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge,
Kazi, Vijana , Ajira na Walemavu) Mhe. Jenista Mhagama alisema
Serikali ya Awamu ya Tano chini ya Uongozi wa Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli
amedhamiria kutokomeza dawa za kulevya hapa nchini.
Wakati huohuo, Waziri wa Habari, Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe.
Harisson George Mwakyembe alisema amefurahishwa na nia njema iliyoonyeshwa na
wasanii ya vita dhidi ya matumizi na biashara ya dawa za kulevya.
No comments:
Post a Comment