Saturday, February 9, 2019

YALIYOJIRI KATIKA UZINDUZI WA KAMPENI YA KUZUIA VIFO VITOKANAVYO NA UZAZI NA WATOTO WACHANGA MKOA WA SONGWE

Mkuu wa Mkoa wa Songwe Brig. Jen. (Mst) Nicodemus Mwangela akisaini mkataba wa kutokomeza vifo vitokanavyo na uzazi na watoto wachanga wakati wa Uzinduzi wa Kampeni ya Jiongeze tuwavushe salama, pembeni yake ni Mkuu wa Wilaya ya Songwe Samuel Jeremia.
Mkuu wa Mkoa wa Songwe Brig. Jen. (Mst) Nicodemus Mwangela akimkabidhi mkataba wa kutokomeza vifo vitokanavyo na uzazi na watoto wachanga Mkuu wa Wilaya ya Momba Juma Said Irando wakati wa Uzinduzi wa Kampeni ya Jiongeze tuwavushe salama.

·        Mkoa wa Songwe umeamua kutokomeza vifo vitokanavyo na Uzazi na Vifo vya watoto wachanga kupitia kampeni ya Jiongeze tuwavushe Salama, maneno basi, sasa vitendo – Mkuu wa Mkoa wa Songwe Brig. Jen. (Mst) Nicodemus Mwangela

·        Takwimu zinaonyesha kuwa bado hatufanyi vizuri katika kutokomeza vifo vya akina mama wajawazito ambapo mwaka 2016 vifo vitokanavyo na uzazi vilikua 26,  huku mwaka 2017 vikiwa 27 na mwaka 2018 ni 32 - Mkuu wa Mkoa wa Songwe Brig. Jen. (Mst) Nicodemus Mwangela

·        Baadhi ya sababu za vifo hivyo vya akina mama wajawazito ni pamoja na kutoka damu nyingi wakati wa kujifungua, kifafa cha mimba, maambukizi ya VVU, upungufu wa damu na kuharibu mimba - Mkuu wa Mkoa wa Songwe Brig. Jen. (Mst) Nicodemus Mwangela

·        Wakuu wa Wilaya wakisimama vema na kuwawajibisha watendaji walioko chini yao tutaweza kupunguza vifo hivi pia wataalamu wa tiba, familia na wananchi wahakikishe mama mjazito anapumzika, anapata chakula kinachostahili na elimu ya masuala ya uzazi - Mkuu wa Mkoa wa Songwe Brig. Jen. (Mst) Nicodemus Mwangela

·        Mkoa unayo kazi kubwa ya kutokomeza vifo hivi na leo tumezindua kampeni hii ambapo wakuu wa Wilaya zote Mkoani Songwe wame saini hati ya makubaliano ya kutoa kipaumbele katika Afya ya Uzazi na Mtoto - Mkuu wa Mkoa wa Songwe Brig. Jen. (Mst) Nicodemus Mwangela

·        Makubaliano hayo yanalenga kuboresha miundombinu ya kutolea huduma za Afya ya Uzazi na Mtoto, kuwezesha asilimia 50 ya vituo vya Afya kutoa huduma ya upasuaji wa akina mama wajawazito na huduma ya damu salama - Mkuu wa Mkoa wa Songwe Brig. Jen. (Mst) Nicodemus Mwangela

·        Kampeni inalenga maeneo tisa ikiwa ni pamoja na kutoa huduma rafiki kwa vijana, elimu na ushauri nasaha, vipimo na matibabu stahiki na kuhakikisha mama mjamzito anajifungulia katika kituo ambacho kina wataalamu wenye ujuzi, vifaa tiba muhimu na dawa- Mganga Mkuu wa Mkoa wa Songwe Dkt Kheri Kagya.

·        Maeneo mengine ni huduma za dharura kwa matatizi yatokanayo na uzazi, damu salama nay a kutosha, ushirikishwaji wa jamii, taarifa ya kifo cha uzazi na mtoto mchanga pamoja na huduma za rufaa - Mganga Mkuu wa Mkoa wa Songwe Dkt Kheri Kagya.

·        Mikakati iliyowekwa ili kufikia malengo hayo imelenga kuboresha huduma kabla ya ujauzito, wakati wa ujauzito, huduma kwa mtoto mchanga, huduma baada ya kujifungua na huduma kwa vijana - Mganga Mkuu wa Mkoa wa Songwe Dkt Kheri Kagya.

No comments:

Post a Comment