Monday, February 25, 2019

REPSSI YAENDELEA NA KAMPENI KUTOKOMEZA MIMBA NA NDOA ZA UTOTONI

Mkurugenzi Mkazi wa Repssi Tanzania, Edwick Mapalala akiongea na vijana kijiweni kuhusu athali za mimbaMkurugenzi Mkazi wa Repssi Tanzania, Edwick Mapalala akiongea na vijana kijiweni kuhusu athali za mimba
Baadhi ya wanafunzi wakimsikiliza Mkurugenzi Mkazi wa Repssi Tanzania, Edwick Mapalala 

Mwandishi wetu, Pwani.

Shirika linalojihusisha na masuala ya kijamii na kisaikolojia kwa watoto (REPPSI) limeendelea kufanya kampeni ya kutokomeza tatizo la ndoa na mimba za utotoni mkoani Pwani.

Kampeni hiyo inafanyika ili kuhakikisha watoto wa kike wanatimiza ndoto zao za kielimu ili kushiriki katika mkakati wa Serikali wa Tanzania ya viwanda.

Akizungumza na wakazi wa Kibiti Mkoani Pwani, Mkurugenzi Mkazi wa REPSI Tanzania, Edwick Mapalala alisema tatizo la mimba na ndoa za utotoni bado kubwa na kwamba linahitaji jitihada za pamoja kupambana nalo.

“Mfano ni hizi kampeni za kutoa elimu na kuihamasisha jamii kumthamini mtoto wa kike zinasaidia kwa hiyo kama tutaendelea nazo jamii itaelewa, watoto watatimiza ndoto zao,” alisema.

Mapalala alisema katika kampeni hizo wanazoshirikiana na Shirika la Pasada linalojihusisha na masuala ya Ukimwi chini ya Kanisa Katoliki Jimbo Kuu la Dar es Salaam na Pwani, vijana hasa madereva bodaboda wamefikishiwa elimu kuhusu thamani ya mtoto wa kike.

Baadhi ya viongozi wa vijiji na kata walikiri kuwa ndoa za utotoni ni changamoto kubwa lakini wanaendelea kupambana nayo.

Mratibu wa Elimu Kata ya Salala, Wilayani Kibiti Erasmus Assenga alisema kwa mwaka huu tu wanafunzi wawili wa Sekondari katika kata hiyo wameacha masomo kwa mimba.

“Kwa hiyo kampeni hii ni muhimu kwa sababu watoto wa kike wenyewe wanafikishiwa elimu, jamii hasa wanaume wanaelezwa na wanajua umuhimu wa kuwathamini,” alisisitiza.

Kwa upande wake Afisa Ustawi wa Jamii wa Pasada Ester Mbwana alisema anaamini kuwa baada ya kampeni hizo kutakuwa na mafanikio makubwa kwa sababu, jamii inaelewa na imekubali kusaidia katika ulinzi wa mtoto.

No comments:

Post a Comment