Saturday, February 23, 2019

CCM WILAYA YA MUFINDI YAVUNJA NGOME YA UPINZANI,YANYAKUA WANACHAMA WAPYA 162

Mwenyekiti wa chama cha mapinduzi ccm Mkoa wa Iringa,Dkt.Abel Nyamahanga akipokea bendera ya chama cha ACT wazalendo kutoka kwa Ambi Daudi ambae ni Katibu wa ACT wazalendo wilaya ya Mufindi aliyejiunga na ccm leo hii katika maadhimisho ya miaka 42 ya kuzaliwa kwa chama cha Mapinduzi ccm.

Maadhimisho hayo yamefanyika kwa wilayani  Mufindi  kwa kushiriki katika shughuli za  kijamii huku Mwenyekiti wa ccm Mkoa wa Iringa akishirikiana na Kaimu katibu wa ccm Mkoa Marco Mbaga,Mkuu wa wilaya ya Mfindi Jamhuri Davidi  pamoja,Wabunge pamoja  na viongozi wa ccm wilaya ya Mufindi,wanachama na wananchi,wameshiriki madhimisho hayo kwa kuchimba msingi wa ujenzi wa vyoo mbora katika shule ya sekondari Upendo,kujenga daraja,kukabidhi mifuko 49 ya saruji  kwa kikundi cha vijana wajasilimali wanaojishughuliisha na utengenezaji  wa tofali katika eneo la soko  la Mafinga Mjini na shule ya sekondari upendo kwa ajili ya kukamilisha ujenzi wa vyoo pamoja pia wamezungumza na walimu wa wilaya ya Mufindi.

Katika maadhimisho hayo  jumla ya wanachama wapya 162 wamejiunga na chama cha mapiduzi ccm,na kusema kuwa wamekunwa na utendaji mzuri wa Rais Magufuli.
(PICHA NA ESTA MALIBICHE)
Mwenyekiti wa ccm Mkoa wa Iringa Dkt. Abel Nyamahanga akivarishwa skuf mara baada ya kuwasili katika ofisi za ccm wilaya ya Mufindi leo asubuhi.
Badhi ya wanachama wapya waliojiunga na chama cha mapinduzi ccm leo katika maadhimisho ya miaka 42 y kuzaliwa ccm,yaliyoadhimishwa wilayani humo.
 Kiongozi wa soko  la Mafinga  akipokea mifuko ya saruji kwa ajili ya  kikundi cha vijana wajasiliamali wanaojishughulisha na utengenezaji wa tofali.
 Mwenyekiti wa ccm Mkoa wa Iringa  Dkt.Abel Nyamahanga pamoja na Mkuu wa wilaya ya Mufindi  Jamhuri Wilium wakichimba msingi kwa ajili ya ujenzi wa vyoo bora katika shule ya sekondari  Upendo iliyopo Mafinga Mjini.
Mwenyekiti wa ccm Mkoa wa Iringa Dk.Abel Nyamahanga akikagua tofali zilizotengenezwa na kikundi cha vjana wa Uvccm ambao  ni wajasilimali  katika eneo la soko la Mafinga Mjini.
 Mwenyekiti wa ccm Mkoa wa Iringa Dkt.Abeil Nyamahanga  akishiriki kutengeneza tofali

No comments:

Post a Comment