Mwenyekiti wa Bodi ya Ushauri wa Wakala wa Uagizaji wa Mafuta kwa Pamoja (PBPA), Dkt Lutengano Mwakahesya, akizungumza katika kikao cha Bodi hiyo na Waziri wa Nishati, Dkt Medard Kalemani (wa Sita kushoto), Naibu Waziri wa Nishati, Subira Mgalu (wa nne kulia), Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati, Dkt Hamisi Mwinyimvua (wa Tatu kulia) na watendaji wengine wa Wizara.
Wajumbe wa Bodi ya Ushauri wa Wakala wa Uagizaji wa Mafuta kwa Pamoja (PBPA) (kushoto) na Watendaji mbalimbali kutoka Wizara ya Nishati (kulia), wakimsikiliza Waziri wa Nishati, Dkt Medard Kalemani wakati wa kikao chake cha Bodi ya PBPA kilichofanyika jijini Dar es Salaam. Kushoto kwa Dkt. Kalemani ni Naibu Waziri wa Nishati, Subira Mgalu.
Na Teresia Mhagama,
Aliyasema hayo jijini Dar es Salaam
wakati wa kikao chake na Wajumbe wa Bodi ya Wakala huo ambapo kikao
hicho kilihudhuriwa na Naibu Waziri wa Nishati, Subira Mgalu, Katibu Mkuu wa
Wizara ya Nishati, Dkt Hamisi Mwinyimvua, Kaimu Kamishna wa Petroli na Gesi,
Mwanamani Kidaya na watendaji wengine wa Wizara. Dkt. Kalemani aliyasema hayo baada ya Kaimu
Mkurugenzi Mkuu wa PBPA, Erasto Simon, kumueleza kuwa, mpaka sasa mafuta yanapokelewa
katika Bandari Tatu tu ambazo ni Dar es Salaam, Mtwara na Tanga.
“Tunataka kila Bandari ifanye kazi ya kupitisha
mafuta mfano ni Bandari ya Bukoba ambapo mafuta yakipokelewa pale
yanaweza pia kusafirishwa kwenda nchini jirani badala ya kusafirishwa kwa njia
ya barabara kutoka jijini Dar es Salaam,” alisema Dkt Kalemani.
Aidha, Dkt Kalemani aliagiza kuwa, Bandari zote
zinazotumika sasa zipokee pia mafuta ya taa kwani wananchi bado wanatumia
mafuta hayo kwa shughuli mbalimbali kwa kuwa usambazaji wa nishati ya umeme
bado haujafikia asilimia 100.
Pia, Dkt Kalemani aliiagiza Bodi ya PBPA
kuhakikisha kuwa ushiriki wa wazawa katika shughuli za uingizaji mafuta
nchini unaongezeka kwa kuwajengea uwezo wa aina mbalimbali ikiwemo
kuwapa elimu kuhusu shughuli hizo.
Kwa ujumla, Dkt Kalemani aliitaka Bodi hiyo kuwa na
mikakati mbalimbali itakayopelekea kampuni nyingi zaidi kushiriki katika kazi ya
uingizaji wa mafuta nchini tofauti na ilivyo sasa ambapo kati ya kampuni 25
zilizosajiliwa, kampuni zisizozidi Saba ndizo zinashiriki katika uletaji wa
mafuta nchini.
Vilevile aliiagiza Bodi hiyo kuhakikisha kuwa,
inasimamia masuala mbalimbali ikiwemo suala la nchi kupata mafuta kwa
wakati huku yakiwa salama, kutokuwepo migogoro katika shughuli za uingizaji
mafuta nchini, kutokuwepo kwa upotevu wa mafuta, mafuta kushushwa ndani ya muda
mfupi mara yanapowasili na kuhakikisha kuwa nchi inakuwa
na mafuta ya ziada katika muda wote.
Kwa upande wake, Naibu Waziri wa Nishati, Subira
Mgalu alitoa angalizo kwa Bodi hiyo kuhakikisha kuwa, kampuni zinazopewa kazi
za uingizaji mafuta nchini zinakuwa na uzalendo na hivyo kuepusha hujuma zozote
zinazoweza kutokea na kusababisha nchi kuwa na upungufu wa nishati hiyo au
kupata mafuta yasiyo salama.
No comments:
Post a Comment