Mkuu wa mkoa wa Rukwa Mh. Joachim Wangabo
amefafanua fursa mbalimbali za uwekezaji zinazopatikana katika Mkoa hasa sekta
ya kilimo kwa wahitimu wa mafunzo kwa vitendo kutoka katika Chuo cha Taifa cha
Ulinzi waliotembelea mkoani hapa ili kujionea maendeleo ya mkoa.
Wahitimu hao kutoka katika nchi kadhaa barani
Afrika wamelenga kutembelea katika viwanda vikubwa vinavypoaptikana katika
mkoa, maeneo ya uwekezaji wa kilimo, kufika kwenye vivutio vya utalii, machimbo
ya makaa ya mawe pamoja na hifadhi za misitu.
Mh.Wangabo alisema kuwa uwekezaji wa kwenye viwanda
unahitajika kwasababu ya uwepo wa mazao ya kulisha viwanda hivyo ikiwemo
viwanda vya kuchakata mahindi, maharage na mpunga na kuwaondoa shaka juu ya
upatikanaji wa umeme kwani hadi kufikia mwaka 2020 vijiji vyote vya mkoa wa
Rukwa vitakuwa na umeme.
“Maeneo mazuri ya uwekezaji upo kwenye viwanda hasa
viwanda vya kuchakata mazao ndani ya mkoa wetu, pia mwaka huu tuna zao la
alizeti kama zao la Kimkakati ambapo hadi sasa kuna tani za mbegu zaidi ya
11,000 ambazo zimeshanunuliwa na wakulima na kupandwa na hivyo tunategemea
uzalishaji mkubwa wa alizeti kwa mwaka huu na hivyo tunawaalika wawekezaji
kuweka viwanda vya uchakataji wa alizeti ikiwa ni zao la kimkakati kwenye mkoa
wetu.” Alisema.
Aidha, alibainisha kuwa katika kuunga mkono juhudi
za serikali ya awamu ya tano, mkoa umejipanga kulima zao la kahawa ambalo ni
moja ya mazao matano ya kimkakati kwa serikali, na kusisitiza kuwa upatikanaji
wa samaki katika ziwa Tanganyika na ziwa Rukwa bado unahitaji uwekezaji ili
kukuza sekta hiyo na hatimae kukuza vipato vya wavuvi wa maeneo ya maziwa hayo,
huku akielezea uboreshwaji wa miundombinu ya barabara na kiwanja cha ndege cha
mkoa.
Ameyasema hayo wakati akijibu swali la Brigedia
Generali Mohamed Montaser muhitimu kutoka nchini Misri aliyetaka kujua maeneo
ya vipaumbele katika uwekezaji kwa mkoa wa Rukwa.
Halikadhalika, Kiongozi wa wahitimu hao Kamishna
Msaidizi Mwandamizi wa Jeshi la Magereza SACP Justine Kaziulaya aliushukuru
uongozi wa Mkoa wa Rukwa kwa mapokezi mazuri waliyoyapata na kuomba kupokewa
tena endapo watarudi Mkoa wa Rukwa katika miaka inayofuata.
Maelezo ya Picha
IMG_5546 - Katibu Tawala wa Mkoa wa Rukwa Benard
Makali (kulia) akipokea moja ya zawadi alizopewa na Uongozi wa chuo cha Ulinzi
nchini ikiwasilishwa na Kiongozi wa Msafara huo Commodore M. Mumanga
IMG_5551 - Picha ya apmoja kati ya Wahitimu wa Chuo
cha Ulinzi nchini pamoja na Wataalamu wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Rukwa
wakiongozwa na Mkuu wa mkoa Mh. Joachim Wangabo (wa tatu toka Kulia).
IMG_55281 - Mkuu wa mkoa wa Rukwa Mh. Joachim
Wangabo (kulia)akipokea moja ya zawadi alizopewa na uong
No comments:
Post a Comment