Na Maiko Luoga
Mbunge wa Jimbo la Serengeti Mkoani Mara Kupitia Chama cha
Mapinduzi CCM Mh. Marwa Ryoba Chacha January 03 Mwaka huu 2019 Alifanya Ziara ya
Kikazi katika Kata ya Matare Ili Kusikiliza Kero za Wananchi na Kuzitafutia
Ufumbuzi.
Ziara hiyo ya Kikazi Iliyofanywa na Mh. Marwa Chacha Ilihudhuriwa
na Wajumbe wa Kamati ya maendeleo ya kata ya Matare KAMAKA wakiongozwa na
Diwani wa Kata hiyo Mh.Nyangi, Wananchi wa Matare Pamoja na Vingozi wa Chama
Cha Mapinduzi CCM na Chama cha Demokrasia na Maendeleo Chadema Ambao
walishuhudia Utekelezaji wa Ilani ya Chama cha Mapinduzi kwa Vitendo.
Akizungumza na Mwandishi wetu Kwa Njia ya Simu Mbunge huyo wa
Jimbo la Serengeti Mkoani Mara Mh. Marwa Chacha Alisema Kuwa Mkutano Mkubwa wa
Hadhara Ulifanyika katika Kitongoji cha Matare Chenye Shule ya Msingi ambayo
Choo chake Kipo katika Hali mbaya hivyo Mbunge huyo Aliamua kuwachangia
wananchi fedha Kiasi cha Tsh. 3,000,000/=ili Kukamilisha Ujenzi wa Choo hicho
cha Wanafunzi.
Aidha Mh. Chacha Alitoa kiasi cha Tsh.2,000,000/= kwa ajili ya
ukamilishaji wa darasa Moja na ofisi ya walimu Katika Shule ya Msingi Igina
Ujenzi ambao wananchi waliuanzisha Kwa nguvu zao wenyewe lakini Haukufika
Mwisho Hivyo Pesa hiyo itawasaidia Kukamilisha Ujenzi Huo Pia Katika Shule Mpya
inayoanzishwa katika Kitongoji cha Kegonga Mbunge huyo Alikabidhi Kiasi Cha
Tsh.5,000,000/= Ili kuwaunga Mkono wananchi Kwaajili ya ukamilishaji wa Majengo
Mawili ya madarasa.
Kuhusu Ushirikiano wake na Wananchi Mh. Marwa Ryoba Chacha Mbunge
wa Serengeti Alieleza Bayana kuwa Ushirikiano Ni mkubwa Hali ambayo Itazaa
Matokeo Mazuri Kwa Chama cha Mapinduzi CCM Jimboni kwake katika Uchaguzi wa
Serikali za Mitaa Utakaofanyika Mwaka huu 2019 Kwakuwa Jimbo Hilo ni la CCM
Tangu yeye Akiwa Chadema Akisema kuwa Hata waliompigia Kura Akiwa Chadema ni
Wanachama wa CCM.
"Nikujulishe Ndg. Mwandishi wa Habari kwamba Kwaasili
Serengeti ni Jimbo la CCM Hata mimi wakati nikiwa Chadema walionipigia kura ni
Wana CCM Ndio maana wakati Nimeamua Kurudi CCM Wananchi walifarijika Sana
lakini Walihuzunika kama kumetokea Msiba wakidhani Sitarudi tena Bungeni
Kutokana na Namna ninavyofanya Kazi kwakushirikiana nao Na walipoona Nimegombea
Tena Kupitia CCM Walinichagua kwa Kishindo Kikubwa Hivyo Nasema Vitongoji na
Vijiji vyote Mwaka huu Vitaenda CCM Naomba hata Mh. Rais Alitambue
hilo".Alisema Mh. Chacha Mbunge wa Serengeti.
Katika hatua Nyingine Mbunge huyo Amesema kuwa CCM yasasa chini ya
Nwenyekiti wake wa Taifa na Rais wa Tanzania Ndg. John Magufuli Imesimama Imara
katika Kutetea Wananchi Ndio maana Watanzania Wanaendelea Kukiamini Chama hicho
Nakuongeza Kuwa Baada ya Bunge Mwezi February Mwaka Huu Atafanya Ziara ya
Kikazi katika Kata zote za Jimbo lake la Serengeti Kuzungumza na Wananchi.
No comments:
Post a Comment