Ni Tunzo nyengine ya heshima ya Kimataifa!
Mtanzania, Mohamed Mansour Nassor anaetokea Zanzibar ambae anafanya masomo kiwango cha juu ya PhD katika fani ya Uchumi ambae pia ndio Raisi wa Umoja wa Vijana na Wanafunzi wa Nchi zote za Afrika(ASSAFSTU) katika Chuo Kikuu kwa Jina maarufu la Patrice Lumumba(RUDN University) ametunukiwa tunzo kubwa ya Kimataifa kwa Kuhamasisha vijana wa nchi za Afrika nchini Urusi.
Na ujumbe wake ulisema kama ifuatavyo:
Leo tarehe 12/01/2019 kwa uwezo wa Mungu nimefikia tena kutambuliwa Kimataifa na najivuna tumeendelea tena kulitangaza vyema Taifa letu la Tanzania katika anga za Kimataifa.
Kwa heshima kubwa kwangu na kwa nchi yetu, nimetunukiwa Tunzo ya kufanya vyema sana katika kuhamasisha vijana wa Afrika nchini Urusi katika masuala ya Taaluma(Elimu) na Maendeleo ya Jamii(Community Development) kupitia Shirika la vijana wa Kiafrika lisilo la Kiserikali(NGO) la Youth of Large Exploit(YOLE) katika hafla yao iliofanyika mjini Moscow.
Aidha licha ya hivyo bado, nimekua nikifanya kazi za uongozi kama Makamu Mwenyekiti wa Diaspora ya Watanzania nchini Urusi na nchi za CIS yani TADIRU na kama Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Kiswahili Cha Moscow(CHAKIMO) chini ya Ulezi wa Balozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Kwa Urusi,Mheshmiwa Simon Marco Mumwi.
Namshukuru sana mheshimiwa Balozi wetu na Ubalozi kwa ujumla kwa mwongozo, nasaha, usahuri na kunipa dira na kunipa msaada mkubwa katika majukumu yangu na harakati zangu.
Nawashukuru sana viongozi wa shirika la YOLE na pia Chama chetu Cha SOYUZ Alumni Association of Tanzania wanaonisahuri sana na pia wao waliniamini ili kuwawakilisha Kimataifa kama Balozi wao tangu waliponiteua mnamo mwaka 2018.
Napenda pia Kukshukuru Chuo Kikuu Changu Kipenzi cha Patrice Lumumba cha Moscow na uongozi wake kwa Kunilea, kunipa fursa mbalimbali na kunipa maarifa na elimu walionipa na nakishukuru pia Chuo Cha Diplomasia cha Tanzania na uongozi wake wote na walimu wangu kwa kunifunza, kunilea na kunipa maarifa zaidi ya masuala ya Mahusiano ya Kimataifa na Diplomasia wakati nilipokua nasoma chuoni hapo mwaka 2016/2017. Kwa hakika mimi ni zao la Chuo Kikuu cha Patrice Lumumba ba pia la Chuo cha Diplomasia.
Napenda kuwashukuru Watanzania wote wanaounga mkono juhudi zangu na harakati zangu na kwa dua zao njema kwangu hasa kwa maslahi mapana ya Taifa letu la Tanzania linaloongozwa na Raisi Makini kabisa, Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli.
Mungu ibariki Afrika, Mungu ibariki Tanzania!
Ahsante sana!
No comments:
Post a Comment