Waziri asiye na wizara maalum Juma Ali Khatib amewataka wakulima kujipanga na kuzidi kuwa karibu na wataalamu wa kilimo ili nguvu za wakulima na mahitaji yao yaweze kuchangia kwa kiasi kikubwa katika kuleta maendeleo ya nchi .
Akiweka jiwe la msingi kituo cha mafunzo ya mbogamboga ,matunda na viungo (taha) waziri huyo huko katika uwanja wa kwa binti hamrani mpendae wilaya ya mjini unguja amesema kuwa endapo kama wakulima hao wataweza kuwa karibu na wataalamu basi wataweza kuzalisha mazao yaliyobora na hata kupata masoko nje ya nchi ya Zanzibar .
Aidha Ndg Juma amesema kuwa kukamilika kwa kituo hicho kutaweza kutimiza mambo ya msingi ikiwemo kuweza kuzalisha zaidi ya mazao ya mbogamboga, kuzalisha matunda kwa wengi na hata hivyo kutoa fursa za ajira kwa vijana waliowengi hapa nchini .
Naibu katibu mkuu wizara ya kilimo maliasili,mifugo na uvuvi Zanzibar ahmad kassim haji ameeleza kuwa wizara ya kilimo itaendelea na juhudi zake za kuelimisha wakulima katika kutunza uzalishaji wa mazao na kuhakikisha kuwa masoko ya uhakikika yanapatikana kwa manufaa ya wakulima .
Akisoma risala ya jumuiya ya Taha meneja wa jumuiya hiyo omari abuubakar mohd amesema kuwa lengo kuu la jumuiya hiyo ni kuweza kutoa taaluma kwa jamii ili waweze kujikita katika masuala ya kilimo hapa nchini .
Akitoa neno la shukrani mkuu wa wilaya ya mjini marina joel Thomas ametoa wito kwa wananchi kudumisha amani na mapinduzi ya nchi na huku akiwataka wanafunzi wa chuo cha kizimbani kuitumia elimu hiyo ipasavyo ili kuweza kujiajiri wenyewe kwa wenyewe na kutongoja ajira kutoka serikalini .
Na ishraa seif ali
No comments:
Post a Comment