Waziri
Mkuu, Kassim Majaliwa akifungua Soko la
Mazao la OTC Lilambo wilayani Songea Januari
3, 2019. Wapili kulia ni Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge,
Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, ambaye pia ni Mbunge wa Peramiho, Jenista
Mhagama, Watatu kushoto ni Waziri wa kilimo, Japhet Hasunga, kushoto ni Mkuu wa
Mkoa wa Ruvuma, Christina Mndeme na kulia ni Mbunge wa Viti Maalum, Jacqueline
Ngonyani Msongozi. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akitazama vyakula mbalimbali vilitokana na unga wa mhogo vilivyoandaliwa na kikundi cha wanamawake wajasiriamali cha Muungano - Mpandagindo, wakati lipofungua Soko la Mazao la OTC Lilambo wilayani Songea, Januari 3, 2019. Kushoto ni Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Jenista Mhagama na kushoto kwa Waziri Mkuu ni Mkuu wa mkoa wa Ruvuma, Christina Mndeme. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akitazama vyakula mbalimbali vilivyoandaliwa na kufungashwa kitaalam na Mtandao wa Wajsiriamali Wadogowadogo Ruvuma (MWARU) wakati alipofungua Soko la Mazao la OTC Lilambo wilayani Songea, Januari 3, 2019. Wapili kushoto ni Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Jenista Mhagama na kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma, Christina Mndeme. Kushoto ni Mkurugenzi wa Mtandao wa MWARU, Lucida Chowo (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akifungua Soko la Mazao la OTC Lilambo wilayani Songea Januari 3, 2019. Wapili kushoto ni Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, ambaye pia ni Mbunge wa Peramiho, Jenista Mhagama, Kulia ni Waziri wa Kilimo, Japhet Hasunga, kushoto ni Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika ya mashariki, Dkt. Damas Ndumbaro, wapili kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma, Christina Mndeme na kulia ni Mbunge wa Viti Maalum, (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
WAZIRI MKUU, Kassim Majaliwa amefungua
mradi wa maghala ya kuhifadhi nafaka na soko la mazao la OTC-Lilambo katika
Halmashauri ya Songea uliogharimu sh. bilioni 1.5.
Amesema
Rais Dkt. John Magufuli ameazimia kuwawezesha wakulima kuwa na mahala pa
uhakika pa kuhifadhia mazao yao na sehemu ya kufanyia biashara ili kuwaongezea
tija.
Amefungua
soko hilo leo (Alhamisi, Januari 3, 2019) akiwa katika siku ya pili
ya ziara yake ya kikazi ya siku nne ya kukagua shughuli za maendeleo mkoani
Ruvuma.
Waziri
Mkuu amesema ameridhishwa na ujenzi wa soko hilo pamoja na maghala kwani
umezingatia viwango. Maghala hayo mawili yana uwezo wa kuhifadhi tani 5,000 za
nafaka.
“Licha
ya soko hili kuwapa wakulima wetu fursa ya kupata masoko ya kuuzia mazao yao,
pia watapata mafunzo ya namna ya kuhifadhi bidhaa zao pamoja na
taarifa za masoko.”
Kadhalika,
Waziri Mkuu ameiagiza bodi ya soko hilo kuhakikisha inatoa matangazo katika
vyombo mbalimbali vya habari ili wakulima waweze kupeleka mazao yao sokoni
hapo.
Wakati
huo huo, Waziri Mkuu amewataka wananchi kutumia vizuri
mvua zinazoendelea kunyesha nchini kuandaa mashamba, kupanda mazao mbalimbali
ya chakula na biashara.
“Nawaagiza
viongozi wa kata na vijiji hakikisheni wananchi katika maeneo yenu wanaandaa
mashamba na kupanda kwa wakati, tunataka tuwe na chakula cha kutosha
na ziada tuuze.”
Awali, Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Wilaya ya Songea, Martin Mtani ameiomba
Serikali iwapatie mashine itakayowawezesha kupanga madaraja ya mazao ya nafaka
mbalimbali.
Mkurugenzi
huyo ameomba soko hilo liwekwe kwenye mpango wa kujengewa vihenge vyenye uwezo
wa kukausha mazao kwa viwango vya kimataifa ili kutatua tatizo la unyaufu.
Pia
Mkurugenzi huyo ameiomba Serikali iwasaidie katika kuliunganisha soko hilo na
TMX ili waweze kuuza mazao ya nafaka ndani na nje ya nchi .
Ufunguzi
huo umehudhuriwa na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Ajira na
Wenye Ulemavu, Jenister Mhagama na Waziri wa Kilimo Japhet Hasunga.
Wengine
ni Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Dkt. Damas
Ndumbaro, Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Christina Mndeme na maafisa wengine wa
Serikali.
No comments:
Post a Comment