Na George Binagi-GB Pazzo
Mbunge wa
Jimbo la Bukombe mkoani Geita, Doto Biteko (CCM), ameunga mkono juhudi za
maendeleo za wakazi wa Kata ya Namonge jimboni humo kwa kuchangia utekelezaji
wa miradi ya maendeleo iliyoanzishwa na wakazi hao.
Akizunguma
kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika katika Kijiji cha Shilabela Novemba 03,
2018, Biteko ambaye pia ni Naibu Waziri wa Madini alichangia mifuko 30 ya
saruji kwa ajili ya kukamilisha ujenzi wa choo katika Shule ya Msingi Shilabela
pamoja na shilingi laki nane kwa ajili ya ujenzi wa choo katika Shule ya Msingi
Nyamagwangala.
Biteko alitumia
mkutano huo kuwapongeza wananchi wa Jimbo la Bukombe kwa kubuni na kutekeleza miradi
mbalimbali ya ya maendeleo na kwamba serikali itaendelea kuwaunga mkono kwani
maendeleo ni ushirika baina ya serikali na wananchi.
Mbunge wa Jimbo la Bukombe mkoani Geita, Doto Biteko (CCM) ambaye pia ni Naibu Waziri wa Madini, akizungumza na wakazi wa Kata ya Namonge kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika Kijiji cha Shilabela.
Tazama Video hapa chini
No comments:
Post a Comment