Saturday, October 13, 2018

MAMBO 7 MUHIMU BAADA YA UZINDUZI MSIMU WA UUZAJI WA KOROSHO 2018/2019 - NACHINGWEA

Wilaya ya Nachingwea imezindua Msimu Wa  uuzaji wa Korosho mwaka 2018/2019 yafahamu MAMBO 7 MUHIMU BAADA YA UZINDUZI MSIMU WA UUZAJI WA KOROSHO 2018/2019 - NACHINGEA yaliyoainishwa na Mkuu wa Wilaya hiyo Mhe Rukia Muwango

1. Marufuku kuuza /kununua nje ya mfumo wa stakabadhi Ghalani(ni kumyonya Mkulima)OCD amejipanga.

2. Makatibu wa vyama Ushirika  (AMCOS) wameapishwa kiapo cha UADILIFU.  Hakimu amejipanga

3. Malipo ya wakulima yatatoka kwa wakati, wakulima wote lazima wafungue akaunti kila mmoja kwa jina lake halisi.  Mameneja wa Benki wamejipanga.

4. Wakulima wamekumbushwa kujiwekea mpango wa matumizi bora ya fedha zao, wanufaike na jasho lao. Kaa mbali na tapeli. 

5. Wameaswa wakulima kutochanganya Korosho na takataka zingine, wahujumu watapata tabu sana. Ubora wa Korosho uzingatiwe.

6. Mnada wa kwanza utaanza Tarehe 24/10/2018 Hapa Nachingwea. Wakulima hudhurieni mkauze Korosho zenu. 

7. Tumegawa vitendea kazi yaani kompyuta, tumegawa kadi za mfuko wa BIMA YA AFYA YA JAMII  (CHF)KWA WAZEE, na tumetoa zawadi mbalimbali kwa washindi wa Michezo.

KOROSHO NI DHAHABU YA KIJANI, UCHUMI WETU TUITUNZE

No comments:

Post a Comment