Saturday, October 13, 2018

JOYCE SIGALLA AWA MGENI RASMI KATIKA MAFUNZO YA VIJANA WA KATA YA MATAMBA

Mafunzo hayo ya siku mbili yaliendeshwa na afisa vijana wa wilaya ya Makete Ndugu Bruno Mwangwale pamoja na afisa elimu watu wazima wilaya ya Makete ndugu Kornel Ntulo.

Bi Joyce Sigalla aliwapongeza vijana hao kwa kufika kwenye mafunzo hayo na kuwataka kuyafanyia kazi mambo yote watakayojifunza.

Pia aliwataka vijana hao kuendana na kasi ya Mheshimiwa Rais Dr John Magufuli kwa kuanzisha viwanda vidogo vidogo katika maeneo yao, na pia kujiunga katika vikundi vya uzalishaji mali.

Wakati wa Mafunzo hao Afisa Vijana wa wilaya hiyo Ndugu Mwangwale aliwafundisha vijana namna ya kubuni na kuendeleza biashara kwa faida zaidi.

Pia afisa elimu watu wazima ndugu Ntulo alisisitiza umuhimu wa kutafuta maarifa kwenye shughuli mbalimbali wanazozifanya ili kuongeza ufanisi zaidi.

No comments:

Post a Comment