Friday, September 7, 2018

DKT TIZEBA AFANYA MAZUNGUMZO NA WATENDAJI WAKUU WA KAMPUNI YA MBOLEA YARA


Waziri wa kilimo Mhe Dkt Charles Tizeba akifanya mazungumzo na watendaji wakuu wa kampuni ya utengenezaji na wasambazaji wa mbolea YARA katika mkutano uliofanyika Mjini Kigali nchini Rwanda jana tarehe 7 Septemba 2018. (Picha Zote Na Mathias Canal-WK)
Waziri wa kilimo Mhe Dkt Charles Tizeba akiagana na watendaji wakuu wa kampuni ya utengenezaji na wasambazaji wa mbolea YARA mara baada ya kumalizika kwa kikao kazi katika mkutano uliofanyika Mjini Kigali nchini Rwanda jana tarehe 7 Septemba 2018.

Na Mathias Canal, Kigali-Rwanda
Waziri wa kilimo Mhe Dkt Charles Tizeba jana tarehe 7 Septemba 2018 amekutana na kufanya mazungumzo na watendaji wakuu wa kampuni ya utengenezaji na wasambazaji wa mbolea YARA.
Katika kikao hicho kilichofanyika katika ulumbi wa mikutano wa kimataifa wa Kigali Convertion Centre uliopo mjini Kigali nchini Rwanda Miongoni mwa mambo yaliyojadiliwa ni pamoja na bei ya mbolea hiyo ikiwa ni pamoja na maswala mazima ya Ubora wake.
Mbolea za YARA zimegawanyika katika makundi makuu matano Yara Mila:  Kundi hili lina aina za mbolea zenye madini makubwa matatu yaani NPK  (Nitrogen, Phosphorus, Potassium), Yara Liva:  Kundi hili lina aina za mbolea zenye asili ya Calcium Nitrate ambazo ni kama vile Nitrabor, Tropicoti na Calicinite, Yara Bela:  Kundi hili ni Kundi lenye mbolea zenye asili ya Ammonium Sulphate Nitrate, zina Nitrojen na Sulphur ambazo ni Sulfan, Yara Vita:  Kundi hili ni la mbolea zile zenye madini yanayohitajika kwa kiwango kidogo na mmea (MicroNutrients) lakini muhimu katika ukuaji wa mmea sambamba na Yara Vera:  Kundi la tano na la mwisho ni mbolea za UREA. 
MWISHO.

No comments:

Post a Comment