Friday, September 7, 2018

DKT TIZEBA AFANYA MAZUNGUMZO NA MKURUGENZI MTENDAJI WA TAASISI YA GLOBAL ENVIRONMENT FACILITY


Waziri wa kilimo Mhe Dkt Charles Tizeba alipokutana na kufanya mazungumzo na Bi Naoko Ishii ambaye ni Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Global Environment Facility (GEF) ya Washington DC nchini Marekani akiwa ameambatana na maafisa wake kutoka GEF, katika mkutano uliofanyika Mjini kigali nchini Rwanda jana 7 Septemba 2018. (Picha Zote Na Mathias Canal)
Waziri wa kilimo Mhe Dkt Charles Tizeba alipokutana na kufanya mazungumzo na Bi Naoko Ishii ambaye ni Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Global Environment Facility (GEF) ya Washington DC nchini Marekani akiwa ameambatana na maafisa wake kutoka GEF, katika mkutano uliofanyika Mjini kigali nchini Rwanda jana 7 Septemba 2018. 

Na Mathias Canal, Kigali-Rwanda

Waziri wa kilimo Mhe Dkt Charles Tizeba jana 7 Septemba 2018 amekutana na kufanya mazungumzo na Bi Naoko Ishii ambaye ni Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Global Environment Facility (GEF) ya Washington DC nchini Marekani akiwa ameambatana na maafisa wake kutoka GEF.

Mazungumzo hayo yametuama kwa masaa kadhaa katika ukumbi wa kimataifa wa mikutano wa Kigali Convention Centre mjini Kigali nchini Rwanda kunakofanyika kongamano la mapinduzi ya kijani Afrika.

Mtendaji Mkuu huyo wa Global environmental Facility (GEF) amemueleza Waziri wa kilimo kuwa hivi karibuni GEF imesimika awamu ya saba ya uwezeshaji kifedha, ambao hujumuisha dola za kimarekani milioni 500 katika nyanja za mifumo ya chakula, matumizi bora na uhuishaji wa ardhi ambapo Kanda ya Afrika ina nafasi kubwa sana kufanya nao kazi katika mradi huo.

Mhe Tizeba alisema kuwa Tanzania ni nchi inayotilia msisitizo katika kilimo na matumizi bora ya ardhi kwa miaka kadhaa hivyo fursa hiyo ni miongoni mwa matakwa ya Tanzania ambayo itawakomboa wakulima nchini Tanzania.

Aliongeza kuwa Tanzania inawasisitiza wananchi kutunza vyanzo vya maji kwani endapo kama visipotunzwa uoto wa asili hususani misitu na hata kilimo kitakuwa mashakani.

MWISHO.

No comments:

Post a Comment