Mkuu wa mkoa Iringa Amina Masenza akiongea na waandishi wa habari ofisini kwake juu ya uzinduzi wa kampeni ya kuhamasisha upimaji wa VVu
Baadhi ya wadau na viongozi wa mkoa wa Iringa waliohudhuria kwenye tukio la uzinduzi wa kuhamasisha upimaji VVU mkoa wa Iringa.
NA FREDY MGUNDA,IRINGA.
SERIKALI ya mkoa wa Iringa
inatarajiwa kuwapima VVUtakribani wananchi elfu tisini (90,000) kwa lengo la
kudhibiti ongezeko la ugonjwa wa ukimwi na kuwaanzishia kutumia ARV KWA wale AMBAO
wamekututwa na VVU.
Hayo yamesemwa na mkuu wa mkoa
wa Iringa Amina Masenza wakati akiongea na waandishi wa habari ofisini kwake,
kwa kusema kuwa kuwa wizara ya afya maendeleo ya jamii jinsia,wazee na watoto
kupitia mpango wa taifa wa kudhibiti UKIMWI kwa kushirikiana na TACAIDS na
wadau wa USAID tulonge afya na kuzinduliwa siku ya tarehe 24 julai 2018 katika
viwanja vya Mwembetogwa.
kamapeni hii itahamasisha
mkakati mpya wa serikali wa upimaji wa VVU na kuanza matumizi ya ARV mapema kwa
wale ambao watakuwa wamekugulika kuwa na maambukizi ya VVU,kupitia kampeni ya “Furahayangu,
pima ujitambue,ishi” ujumbe huo mutakufanya mtu uliyepima kuwa huru. Alisema Masenza.
Masenza alisema kuwa serikali
ya awamu ya imedhamilia kuhakikisha kuwa inapambana kuhakikisha inapunguza
maambukizi ya ukimwi na kufikia lengo la “TISINI TATU” ifikapo mwaka 2020 na
wananchi asilimia tisini wawe wamejua hali zao za maambukizi na wawe wamepimwa
VVU ILI waweze kupatiwa dawa za kupunguza makali ya VVU.
Aidha Masenza alisema kuwa
serikali ya mkoa wa Iringa umejipanga kuhakikisha vitendanishi na dawa ARV zipo
za kutosha katika kila kituo kinatoa huduma ili kuweza kuwahudumia vizuri na
kuwaanzishia dawa watakagundulika kuwa na maambukizi ya VVU na Ukimwi.
Masenza alisema kuwa serikali ya
mkoa imevitaka vyombo vya habari mkoani hapo kushiriki kuhamasisha jamii
Hivyo
aliwataka wananchi kujitokeza kwa wingi kushiriki maandamano yatakayoanzia
bustani ya Manispaa kisha uwanja wa Mwembetogwa.
Alisema
kuwa mwandishi bora atapewa zawadi kulingana na vigezo vitakavyo wekwa.
No comments:
Post a Comment