Waziri wa kilimo Dkt Charles Tizeba akisisitiza umuhimu wa ushirika kwenye sherehe za siku ya kilimo biashara kwa wadau wa kilimo inayofanywa kwa pamoja na Taasisi ya utafiti wa kilimo TARI-SERIAN na baraza la nafaka Ukanda wa Afrika Mashariki (EAGC) katika viwanja wa Taasisi ya utafiti SERIAN Mjini Arusha jana tarehe 20 Julai 2018. (Picha Zote Na Mathias Canal-WK)
Waziri wa kilimo Dkt Charles Tizeba akisisitiza jambo mara baada ya kutembelea shamba la maonesho ya mahindi kwenye sherehe za siku ya kilimo biashara kwa wadau wa kilimo iliyofanyika jana jana tarehe 20 Julai 2018 katika viwanja wa Taasisi ya utafiti SERIAN Mjini Arusha.
Waziri wa kilimo Dkt Charles Tizeba akisisitiza jambo mara baada ya kutembelea shamba la maonesho ya vitunguu kwenye sherehe za siku ya kilimo biashara kwa wadau wa kilimo iliyofanyika jana jana tarehe 20 Julai 2018 katika viwanja wa Taasisi ya utafiti SERIAN Mjini Arusha.
Waziri wa kilimo Dkt Charles Tizeba akisisitiza umuhimu wa ushirika kwenye sherehe za siku ya kilimo biashara kwa wadau wa kilimo inayofanywa kwa pamoja na Taasisi ya utafiti wa kilimo TARI-SERIAN na baraza la nafaka Ukanda wa Afrika Mashariki (EAGC) katika viwanja wa Taasisi ya utafiti SERIAN Mjini Arusha jana tarehe 20 Julai 2018.
Waziri wa kilimo Dkt Charles Tizeba akiwa katika picha ya pamoja na Mtendaji Mkuu EAGC, Mtendaji Muu wa TARI, Mawakala wa pembejeo za kilimo, Watafiti na viongozi mbalimbali wa Mkoa wa Arusha mara baada ya kuhutubia mamia ya wananchi kwenye sherehe za siku ya kilimo biashara kwa wadau wa kilimo katika viwanja wa Taasisi ya utafiti SERIAN Mjini Arusha jana tarehe 20 Julai 2018.
Na
Mathias Canal-WK, Arusha
USHIRIKA ni dhana ya kuleta
maendeleo kwa kushirikiana, Dhana hii imefanikiwa kuleta mabadiliko ya kiuchumi
na kijamii katika kipindi cha miaka kadhaa iliyopita, Kutokana na changamoto
mbalimbali zilizoikumba sekta hii ya ushirika watu wengi walikosa imani na
vyama hivyo kutokana na viongozi wake kutokuwa waaminifu (Wabadhilifu).
Ni wazi kuwa katika kipindi cha
miaka miwili hivi, imani kwa vyama vya ushirika imeongezeka na vyama vingi
vinaendelea kuundwa hasa vile vya kuweka na kukopa, yaani SACCOS.
Waziri wa kilimo Dkt Charles Tizeba ameyasema hayo jana 20 Julai 2018 wakati wa hotuba yake katika siku ya
kilimo biashara kwa wadau wa kilimo inayofanywa kwa pamoja na Taasisi ya
utafiti wa kilimo TARI-SERIAN na baraza la nafaka Ukanda wa Afrika Mashariki
(EAGC).
Alisema kuwa uanzishwaji wa
vyama vingi vya ushirika kwa sasa unatokana na elimu watu wengi waliyoipata
kuhusu Ushirika na watu kuendelea kuelewa kuwa changamoto zilizoko ndani ya
ushirika zinatatulika ikiwa ni pamoja na hivi karibuni kutangaza kiama kwa
baadhi ya viongozi wabadhilifu wa vyama hivyo ambao wanautumia ushirika kama
sehemu ya kujinufaisha wao pasina kuwa na mtazamo wa mafanikio kwa wanachama
wote.
Alisema, Dhamira ya Ushirika ni
nzuri na kama itafanya kazi vizuri ni njia nzuri ya kuleta mabadiliko kwa watu
wengi huku akisisitiza Wanachama wa Ushirika kujiimarisha katika misingi ya
uaminifu, uwazi, uwajibikaji kwa jamii na kuwajali wengine.
Dkt Tizeba alisema Ushirika ni
muungano wa watu ambao wanafanya kazi pamoja kwa hiari ili kufanikisha mahitaji
yao ya kiuchumi, kijamii na kiutamaduni kupitia shughuli ya biashara
inayomilikiwa kwa pamoja na kudhibitiwa kidemokrasia kwani njia pekee yenye
tija na mafanikio ya kilimo kwa mkulima ni kuuza mazao yao kupitia mfumo huo
rasmi wa ushirika.
“Kupitia ushirika kutamfanya
mkulima kujihami na bei kwa kuuza kwa pamoja kwani kwa muda mrefu kilimo cha
masoko kimekuwa kikitengenezwa na wakulima wenyewekwa sababu ya kutojiunga pamoja
na kuwa na mfumo rasmi” Alikaririwa Dkt tizeba na kuongeza kuwa
“Kunapokuwa na chama imara cha Msingi,
chama hiki kinaunda chama kikuu kilicho imara kwa kufanya hivyo tutaondokana na
uduni wa bei kwa mkulima kutokana na kushuka bei kwa mazao kwa sababu ya
mkulima mmoja mmoja kuuza mazao yake mwenyewe” Alisema
Waziri huyo wa kilimo Mhe Dkt. Charles
Tizeba alisema Serikali imeamua kufufua ushirika kwa sababu ndiyo mkombozi wa
wakulima. "Tumeamua kurudisha ushirika aminifu kwa wakulima, na nirudie
kutoa onyo kwa viongozi waliopata dhamana ya kuongoza ushirika wasidhani kule
wameenda kupata ulaji.” Alisema
Alisema kuwa pamoja na kwamba serikali
inatambua kuwa ushirika ni nyenzo muhimu ya kuwasaidia wananchi katika
upatikanaji wa mtaji na kuwawezesha kuunganisha nguvu zao za katika
kujiendeleza kiuchumi lakini kuongezwa somo la ushirika kwenye mtaala wa elimu
italeta mageuzi makubwa kwa wakulima.
Alisema kuwa pamoja na juhudi
kubwa zinazofanywa na serikali kwa kushirikiana na wadau mbalimbali ili
kuhakikisha wananchi wengi zaidi wanahamasishwa na hatimae kujiunga kwenye
vyama vya ushirika kulingana na shughuli zao za kiuchumi ili kuondoa
dhana ya kudhani kwamba vyama vya ushirika ni kwa ajili ya Kilimo cha
Mazao ya biashara ya nchi za nje lakini juhudi hizo zitakuwa na mabadiliko
chanya zaidi kama ushirika utafundishwa mashuleni.
MWISHO.
No comments:
Post a Comment