Waziri wa Kilimo Mhe Dkt Charles Tizeba akihutubia mamia ya wananchi waliojitokeza kwenye sherehe za Siku ya Kilimo Biashara kwa wadau wa kilimo iliyofanyika kwa pamoja na Taasisi ya utafiti wa Kilimo TARI-SERIAN na Baraza la nafaka Ukanda wa Afrika ya Mashariki (EAGC) katika viwanja vya Serian mjini Arusha, Jana tarehe 20 Julai 2018. (Picha Zote Na Mathias Canal-WK)
Baadhi ya wakilima wakifatilia hotuba ya Waziri wa Kilimo Mhe Dkt Charles Tizeba wakati akihutubia kwenye sherehe za Siku ya Kilimo Biashara kwa wadau wa kilimo iliyofanyika katika viwanja vya Serian mjini Arusha, Jana tarehe 20 Julai 2018.
Waziri wa Kilimo Mhe Dkt Charles Tizeba akizungumza na wafanyabiashara wa mazao mbalimbali alipowatembelea kwenye banda la mafunzo wakati wa sherehe za Siku ya Kilimo Biashara kwa wadau wa kilimo iliyofanyika kwa pamoja na Taasisi ya utafiti wa Kilimo TARI-SERIAN na Baraza la nafaka Ukanda wa Afrika ya Mashariki (EAGC) katika viwanja vya Serian mjini Arusha, Jana tarehe 20 Julai 2018.
Waziri wa Kilimo Mhe Dkt Charles Tizeba akihutubia mamia ya wananchi waliojitokeza kwenye sherehe za Siku ya Kilimo Biashara kwa wadau wa kilimo katika viwanja vya Serian mjini Arusha, Jana tarehe 20 Julai 2018.
Mtafiti Mkuu wa kituo cha utafiti wa kilimo SERIAN Dkt John Saria akimueleza Waziri wa Kilimo Mhe Dkt Charles Tizeba umuhimu wa mashine ya kupandia Mahindi, Maharage, Alizeti, na Mbaazi kwenye sherehe za Siku ya Kilimo Biashara kwa wadau wa kilimo iliyofanyika katika viwanja vya Serian mjini Arusha, Jana tarehe 20 Julai 2018.
Na Mathias Canal, Arusha
Waziri wa Kilimo Mhe Dkt Charles Tizeba ameiagiza Taasisi ya
udhibiti wa Ubora wa mbegu (TOSCI) kukutana na kufanya mazungumzo na
wafanyabiashara wa mbegu Tanzania (Tanzania Seed Trade Association-TASTA) leo
21 Julai 2018 ili kujadili namna ya kupunguza gharama za uuzaji wa mbegu jambo
litakaloongeza tija na unafuu wa bei kwa wakulima.
Waziri Tizeba ametoa agizo hilo Jana tarehe 20 Julai 2018 wakati
akihutubia mamia ya wananchi waliojitokeza kwenye sherehe za Siku ya Kilimo
Biashara kwa wadau wa kilimo iliyofanyika kwa pamoja na Taasisi ya utafiti wa
Kilimo TARI-SERIAN na Baraza la nafaka Ukanda wa Afrika ya Mashariki (EAGC)
katika viwanja vya Serian mjini Arusha.
Agizo hilo linajili Mara baada ya wakulima kulalamika mbele ya
Waziri huyo wa kilimo kuhusu gharama za mbegu kuwa juu mara baada ya kupata
fursa ya kuuliza maswali katika mkutano huo ambapo pamoja na mambo mengine
wananchi hao walimpongeza Mhe Tizeba kwa maagizo hayo.
"Nimemuona hapa Mwenyekiti wa wafanyabiashara wa mbegu
Tanzania (TASTA) Bwana Bobu Shuma akijaribu kuhalalisha bei ya mbegu kwamba ni
rafiki kwa wakulima wetu siwezi kukubaliana naye na haiwezekani serikali
imefuta kodi zote kwenye mbegu lakini wakulima bado wanatozwa kiasi kikubwa cha
fedha hivyo ni lazima mpunguze bei" Alisisitiza Mhe Tizeba
Aliongeza kuwa endapo wafanyabiashara hao watashindwa kupunguza
bei serikali itarejesha kodi zote kwenye mbegu ama kuwafutia leseni baadhi ya
wafanyabiashara watakaoshindwa kufuata na kutekeleza maagizo ya serikali .
"Natoa Siku moja kuanzia sasa mpaka kesho jioni (Leo) kwa TOSCI
na TASTA mkutane mjadiliane majibu mnipatie kabla sijaondoka Arusha kwamba
mmepunguza gharama za mbegu mkishindwa kufanya hivyo mtakuwa mmekiuka matakwa
ya utaratibu wa serikali" Alikaririwa Mhe Tizeba
Katika hatua nyingine Mhe Tizeba amewasihi wafanyabiashara wa
mbegu nchini kuuza mbegu zinazozalishwa nchini badala ya kushadadia mbegu
zinazozalishwa nje ya nchi huku akiongeza kuwa sio lazima kila mzalishaji wa
mbegu azalishe mbegu za nje kwani kufanya hivyo kunawanufaisha wamiliki wa lebo
za mbegu hizo kilimo na kuongeza faida kubwa kwa nchi zingine.
Sambamba na hayo Waziri wa Kilimo Mhe Dkt Charles Tizeba
ameiagiza Taasisi ya udhibiti wa Ubora wa mbegu (TOSCI) kufanya utafiti wa mara
kwa mara ili kujiridhisha kama mbegu zinazotolewa kwa wakulima ni sahihi ama
vinginevyo.
Aidha, ameushukuru uongozi na wataalamu wa utafiti SERIAN,
uongozi wa wafanyakazi wa Baraza la Nafaka Ukanda wa Afrika ya Mashariki,
uongozi na watumishi wa makampuni ya pembejeo kama SEEDCO, Zambia, ETG, PANNAR,
KIBO, MERU, SYGENTA, MONSANTO, SUBA AGRO, MAMS, EAST WEST SEED, Kampuni ya
mbolea YARA na ETG kwa kushiriki kikamilifu kuonyesha aina za mbegu zenye Mazao
mengi.
Katika maonesho hayo mbegu za maharage, Mahindi, soya, Ngano,
shairi, mbaazi, aliseti na mazao ya mbogamboga zilionyeshwa huku wananchi
wakipata fursa ya kujifunza mbinu bora za kilimo ikiwa ni pamoja na kuunganisha
uelewa wa pamoja na wataalamu wa mazao hayo
MWISHO
No comments:
Post a Comment