Tuesday, January 9, 2018

NAIBU WAZIRI WA UCHUKUZI ATEMBELEA JIMBO LA ILEMELA

Naibu Waziri wa Uchukuzi na Mawasiliano Mhe Mhandisi Atashasta Nditie ametembelea Jimbo la Ilemela kujionea changamato za mawasiliano zinazolikabili Jimbo hilo hasa maeneo ya Visiwani na nje ya Mji kufuatia ombi la Mbunge wa Jimbo la Ilemela  Mhe Dkt Angeline Mabula

Akiwa Jimboni humo Mhe Mhandisi Nditie  amefika kata za Sangabuye na Kayenze na kujionea kero  na changamoto ya kimtandao inayowakabili wananchi wa maeneo hayo na kusababisha kukosekana kwa mawasiliano ya uhakika kunakopelekea kukwama kwa shughuli za maendeleo ambapo amewahakikishia wakazi wa maeneo hayo juu ya kutafuta ufumbuzi wa kudumu kumaliza kabisa changamoto hiyo inayowakabili

Kwa upande wake Mbunge wa Jimbo la Ilemela ambae pia ni Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe Dkt Angeline Mabula mbali na kumshukuru Naibu Waziri huyo kwa kutembelea Jimbo la Ilemela ameongeza kuwa ziara aliyoifanya  Naibu Waziri huyo ni matokeo  ya Ombi lake la kumtaka kuja kujionea hali halisi yachangamoto ya  kimawasiliano wanayoipata wananchi wake  huku akiwataka wananchi na viongozi kuendelea kushikamana na  kushirikiana katika kufikia malengo ya Serikali ya awamu ya Tano chini Mhe Rais Dkt John Magufuli

‘… Ziara hii ya Naibu Waziri wa Uchukuzi na Mawasiliano ni matokeo ya ombi langu nililomuamba kufika katika Jimbo langu ili ajionee changamoto na kero ya mawasiliano wanayoipata wananchi wangu hasa wa pembezoni mwa mji na wale wanaoishi maeneo ya Visiwani kikiwemo kisiwa cha Bezi ili na wao wakae waone wanaweza kutusaidiaje kumaliza changamoto hii …’ Alisema Mhe Dkt Angeline

Katika ziara hiyo Mhe Mhandisi Atashasta  Nditie aliambatana na wataalamu kutoka wizara yake na wataalamu kutoka Kampuni ya Simu za Mkononi ya Halotel ambao wameahidi kujenga mnara wa Simu ili kuhakikisha yanakuwepo mawasiliano ya uhakika kwa wananchi wa maeneo hayo

‘ Ilemela ni yetu, tushirikiane kuijenga ’

Imetolewa na
Ofisi ya Mbunge
Jimbo la Ilemela
09.01.2018

No comments:

Post a Comment