Naibu Waziri wa Wizara ya Maji na Umwagiliaji Mhe Juma Aweso akijaribu kuendesha baiskeli yenye madumu ya maji ili kujionea kwa vitendo namna ambavyo wananchi wanakumbwa na adha hiyo wakati wa ziara yake ya kikazi Mkoani Shinyanga Jana 10 Januari 2018.Baadhi ya wananchi wakizungumza na Naibu Waziri wa Wizara ya Maji na Umwagiliaji Mhe Juma Aweso kufikisha malalamiko yao kuhusu kadhia ya maji wakati wa ziara yake ya kikazi Mkoani Shinyanga Jana 10 Januari 2018.
Na Mathias Canal, WazoHuru Blog
Naibu Waziri wa Wizara ya Maji na Umwagiliaji Mhe Juma Aweso amezuru Mkoani Shinyanga Jana 9 Januari 2018 kwa ajili ya kukagua miradi mbalimbali ya maji Mkoani humo ili kuona ufanisi wa utendaji na utekelezwaji wa ilani ya uchaguzi ya CCM mwaka 2015-2020.
Akiwa Katika Wilaya ya Shinyanga Vijijini Mhe Aweso amewasisitiza wananchi kuendelea kutoa ushirikiano wa karibu kwa serikali ili ukamilifu wa miradi mbalimbali ya maji nchini uwe katika muktadha mpana na mafanikio kwao.
Akizungumza katika ziara hiyo Mhe Aweso amesisitiza kuwa serikali ya awamu ya Tano inayoongozwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Dkt John Pombe Magufuli imekusudia kuboresha huduma za wananchi ikiwemo urahisi wa upatikanaji wa maji safi na salama hivyo ni jukumu lao kuunga mkono juhudi hizo za serikali.
Alisema kuwa Wizara yake itahakikisha maji safi na salama yanapatikana kama ambavyo ilani ya uchaguzi inaelekeza.
Aidha, Mhe Aweso amekerwa na jinsi utekelezwaji wa miradi ya Maji Wilayani Shinyanga unavyochechemea jambo ambalo linarudisha nyuma ufanisi wa upatikanaji wa maji kwa wakati.
"Tumekuta miradi imechelewa kumalizika tangu mwaka 2014 mpaka Mwaka huu 2018 inaelekea miaka minne sasa, changamoto ni wakandarasi ambao hawana uwezo wa kifedha na wakipewa pesa wanatumia kwa matumizi mengine na kufanya mradi uchelewe huku makubaliano yalitakiwa kufika ukomo mwezi wa 4 mwaka jana" Alikaririwa Mhe Aweso
Naibu Waziri wa Wizara ya Maji na Umwagiliaji Mhe Juma Aweso ameanza Jana 9 Januari 2018 ziara ya kikazi ya siku tatu Mkoani Shinyanga ambapo itamalizika Jumamosi 12 Januari 2018
MWISHO
No comments:
Post a Comment