Mbunge wa jimbo la Mufindi
KaskaziniMahamuod Mgimwa akizungumza na wananchi katika moja ya shule ambayo inahitajika kujengewa vyumba viwili ya madarasa na kukarabati vyumba vingine vitatu kwa gharama za wananchi na mbunge mwenyewe akichangia kwa asilimia kubwa kuboresha maendeleo ya sekta ya elimu kwa wananchi na wanafunzi wa jimbo hilo
Mbunge wa jimbo la Mufindi
KaskaziniMahamuod Mgimwa akizungumza mmoja ya walimu pamoja viongozi kutoka kwenye ofisi yake ya mbunge ambao alikuwa ameongoza nao katika kukagua na kutatua changamoto za wananchi kwenye kata ya Kibengu
Mbunge wa jimbo la Mufindi
KaskaziniMahamuod Mgimwa akitoa mfano wa kufanya kazi kwenye ujenzi wa vyumba vitatu vya shule ya msingi Kibengu ambako nako wananchi wamechangia nguvu zao
Katibu wa vijana wa chama cha mapinduzi UVCCM wilaya ya Mufindi akiwa na katibu wa mbunge idara ya uhamasishaji na michezo Lwimbo nao wakijumika na wananchi katika ujenzi wa shule ya msingi Kibengu
Mbunge wa jimbo la Mufindi
KaskaziniMahamuod Mgimwa akizungumza na viongozi katika eneo ambalo vyumba vitatu vya madarasa vinajengwa
Mbunge wa jimbo la Mufindi
KaskaziniMahamuod Mgimwa akizungumza kwenye eneo ambalo ofisi ya kijiji inajengwa ajili ya kurahisisha kutoa huduma kwa wananchi
Mbunge wa jimbo la Mufindi
KaskaziniMahamuod Mgimwa akiwa na diwani wa kata ya Kibengu Zakayo Kilyenyi sambamba na katibu wa mbunge idara ya uhamasishaji na michezo Lwimbo
Na Fredy Mgunda, Iringa
Mbunge wa jimbo la Mufindi
Kaskazini kwa kushirikiana na wananchi wa kijiji cha Kibengu wametumia jumla ya
shilingi milioni mia moja kumi na tisa na laki mbili (119,200,000) katika
ujenzi wa madarasa ya shule,zahanati na nyumba za wafanyakazi wa zahanati na
walimu wa shule zilizopo katika kijiji hicho lengo likiwa katika kuboresha
sekta ya elimu na afya kwa wananchi.
Akizungumza na wananchi katika
kijiji hicho mbunge wa jimbo la Mufindi Kaskazini Mahamuod Mgimwa alisema kuwa
ameamua kuwekeza katika elimu na afya kwasababu wananchi wakifanikiwa kupata
vitu hivyo viwili kwa wakati watafanya maendeleo kwa kasi kubwa kulingana na
wakati uliopo na kuendana na mazingira wanayoishi.
“Hivi ndio vipaumbele vyangu
kwa kijiji hiki kwa wakati huu maana nimegundua kuwa changamoto kubwa ni kuwa
shule nyingi za msingi zilijengwa miaka mingi iliyopita sasa zimechakaa na sio
rafiki kwa wanafunzi kuwasaidia kupata elimu bora hivyo nimeanza na hilo pamoja
na kuchangia maendeleo kwa kuboresha sekta ya afya ili wananchi wakiugua waweze
kutibia hapa hapa kijiji kwa kuwa nina uhakika huduma itakuwa inatolewa kwa
ustadi mkubwa na yenye ubora unaotakiwa” alisema Mgimwa
Mgimwa alieleza kuwa pesa hiyo
itatumika katika maeneo yafuatayo ujenzi wa ofisi ya kijiji cha Kibengu
utatumia gharama ya shilingi milioni thelathini (30,000,000) hadi kukamilika
kwake,kuingiza umeme zahanati na kwenye nyumba za waganga imegarimu kiasi cha
shilingi 1,200,000/=,ujimbaji wa kisima shilingi 2,00,000/=,ujenzi wa nyumba za
walimu mbili kwa moja itagharimu kiasi cha shilingi 25,000,000/= na shule ya
msingi Kibengu kutafanyika ujenzi wa madarasa matatu ambayo yatagharimu kiasi
cha shilingi 21,000,000/=.
“Hizi ni gharama katika
kijijicha Kibengu ambazo nimechangia na wananchi wangu hivyo napenda kuwapa
habari vijiji na vitongoji vingine kwenye jimbo langu kuiga mfano wa kijiji cha
Kibengu na kitongoji cha Mitanzi kwa kujituma kuleta maendeleo” alisema Mgimwa
Aidha Mgimwa alisema kuwa
wananchi wa kitongoji cha Mitanzi katika kijiji cha Kibengu nao wamekuwa
wakitoa ushirikiano na kufanikisha kufanya maendeleo katika maeneo yafuatayo
ujenzi wa nyumba za walimu na madarasa ya shule ya msingi Mitanzi utagarimu
kiasi cha shilingi milioni kumi na saba (17,000,000) uchimbaji wa kisima shilingi 1,000,000/=, ukarabati wa madarasa
mawili shilingi 17,000,000 kutona na yalivyo haribika, kuingiza umeme kwenye
nyumba za walimu na madarasa shilingi 5,000,000/=
“Ukaingalia tumetumia nguvu
kubwa na wananchi kufanikisha haya japo kuna maeneo bado hatujamalizia na
ninauhakika tutamalizia lakini bado kunawatu wanasema eti sifanyi kazi sasa
sijui wataka niwe ninawapa pesa mikononi mwao ili wajue maendeleo yapo” alisema
Mgimwa
Mgimwa alimalizia kwa kuwaomba
wananchi wa jimbo la Mufindi Kaskazini kuendelea kumuunga mkono katika kuleta
maendeleo kwa wananchi wa jimbo hilo kwa kuwa wanajinea kazi anayoifanyia hivyo
wasikubali kulishwa maneno na watu wasiopenda maendeleo.
Kwa upande wake mtendaji wa
kijiji cha Kibengu Dominicus Nyaulingo alimshukuru mbunge wa
jimbo la Mufindi Kaskazini kwa jitihada zake za kuleta maendeleo kwa
kushirikiana na wananchi na kahidi kuwa watandelea kuzitangaza kazi
anazozifanya ili wananchi wote wajue anafanya kazi gani na kupunguza maneo
ambayo yamekuwa yakisemwa bila kuwa na ushaidi juu ya utendaji wa mbunge huyo.
“Kweli kabisa mbunge wetu
amekuwa akifanya kazi kubwa sana ila sisi tumekuwa hatuzisemi kazi za mbunge
kwa wananchi hivyo kuchochea chuku baina ya wananchi na mbunge hivyo kuanzia
leo nitakuwa ninazisemea kazi za mbunge kila kwenye mkutano wa kijiji” alisema Nyaulingo
No comments:
Post a Comment