Mamlaka ya
Chakula na Dawa, TFDA imewakutanisha wajasiriamali wanaosindika chakula mkoani
Geita na kutoa mafunzo yatakayowasaidia kutengeneza vyakula vinavyokidhi
viwango vya usalama na vitakavyoweza kukuza soko la ndani na nje.
Akizungumza
kwenye mafunzo hayo Kaimu Mkurugenzi wa usalama wa chakula makao makuu ya TFDA
Bw Lazaro Mwambole alisema tafiti walizofanya zimebaini kuwa wengi wenye
viwanda vya kusindika chakula hawana vitabu vinavyohusu bidhaa wanazotengeneza
na hawajui kanuni za usindikizaji.
“Mgeni Rasmi
taifiti ambazo zilifanyika mwaka 2016 zilionekana kuwa wamiliki wengi wa viwanda
vya kusindika chakula hawana vitabu vinavyohusu bidhaa wanazozitengeneza hali
ambayo imesababisha kutokufanya kwa ubora zaidi usindikaji wao”Alisema
Mwambole.
Katibu
tawala Msaidizi wa Mkoa wa Geita Bw Emily Kasaga amewaasa wafanyabiashara
kuhakikisha wanarutubisha vyakula ili view salama na vyenye ubora kwa kuwa afya ya
watumiaji iko mikononi mwao.
Baadhi ya
washiriki wa mafunzo hayo Bi Fatma Hassan na Bw Edward Geni wamesema mafunzo
hayo yamewafungulia mwanga zaidi kwa kuwa wengi walikuwa wakifanya kazi hizo
bila kujua kamawanakosea.
No comments:
Post a Comment