Mkuu wa wilaya ya Mufindi
Jamhuri William aliwakata wanajumuiya ya hifadhi ya wanyamapori WAGA kuzitunza rasilimali za wanyama pori kwa faida ya sasa na vizazi vijavyo kama wao walivyotunziwa na wananchi waliokuwepo miaka ya huko nyuma
Mratibu wa shughuli za uhifadhi kwa jamii katika shirika lisilo la
kiserikali (WCS) Anna Kimambo alisema lengo la shirika hilo ni kuhakikisha jamii
zinasimamia vilivyo rasilimali za wanyama pori,misiti na vyanzo vya maji ili
baadae weweze kuona faida ya vitu wanavyo vitunza.
Na Fredy Mgunda,Mbalali
Shirika lisilo la kiserikali
linalojishughulisha na uhifandhi shirikishi wa wanayama pori (WCS) limeipiga
msasa jumuiya ya hifadhi ya wanyamapori WAGA kwa lengo la kuhakikisha kuwa
wanawalinda wanyama pori na kunufaika na uwepo wa wanyama pori hao.
Akizungumza wakati wa mafunzo hayo mkuu wa wilaya ya Mufindi
Jamhuri William aliwakata wanajumuiya ya hifadhi ya wanyamapori WAGA kuyatumia
vizuri mafunzo waliyopata kulinda rasilimali za wanyama pori.
“Nawaombeni tumieni vizuri
mafunzo haya kwa kuwa yatawasidia katika swala zima la uhifadhi ambalo ndio
jukumu lenu la kwanza kabla hamjaangalia nini mnapata kama faida kwa kufanya
hivyo WAGA itakuja kuwa jumuiya kubwa sana” alisema William
William
aliwaomba jumuiya hiyo kutojihusisha na ujangili kwa kuwa wanaelimu ya uhifadhi
na kuhakikisha wanyama pori wanalindwa kwa faida za taifa.
“Kuna
jumuiya nyingi zimekuwa na migogoro kutokana na baadhi ya wajumbe kujihusisha
na ujangili na kusababisha wanyamapori wengi kukimbia katika maeneneo ya
hifadhi na kuwapunguzia kipato kwa wanajumiya hivyo nendeni mkatoe elimu kwa
wananchi wengine kwa kuwa nyinyi mshapata elimu hiyo” alisema William
Aidha
William alisema kuwa jumuiya ya WAGA bado ni changa hivyo wanatakiwa kuheshimu
utawala bora ili kufikia malengo ambayo wamejiwekea kwa kunufaika na pori
ambalo serikali imewapatia kwa ajili ya kufanya maendeleo ya vijiji.
“Najua
kuwa mmeenda kujifunza kwenye jumuiya nyingine na mmeona kuna jumuiya
zinamigogoro mingi hadi serikali huwa inaingilia kati na kuna jumuiya ambazo
zinaendeshwa kwa kufuata utawala bora hivyo nawaomba mjifunze kufanya kazi kwa
kufuata utawala bora” alisema William
William
alilipongeza Shirika lisilo la kiserikali linalojishughulisha na
uhifandhi shirikishi wa wanayama pori (WCS) kwa mikakati wanayoifanya ya kuhaikisha
jumiya ya WAGA inaendeshwa kisasa kwa manufaa ya taifa kwa kulinda wanyama pori
ambao ndio hazina ya taifa katika kukuza pato la taifa.
Kwa
upnde wake mratibu wa shughuli za uhifadhi kwa jamii katika shirika lisilo la
kiserikali (WCS) Anna Kimambo alisema lengo la shirika hilo ni kuhakikisha jamii
zinasimamia vilivyo rasilimali za wanyama pori,misiti na vyanzo vya maji ili
baadae weweze kuona faida ya vitu wanavyo vitunza.
“Unajua
kila siku nasema kuwa mtu akitunza rasilimali za wanyama pori nauhakika faida
yake ni rahisi kuipata kutoka na kupata wawekezaji wengi ambao watakimbila eneo
hilo kwa kuwa limehifadhiwa vizuri na litakuwa na wanyama pori wengi” Kimambo
Kimambo
alisema kuwa WCS iliamua kuanza kuisaidia jumuiya hii ya WAGA kwa kutumia fedha
za msaada kutoka USD ambazo zimetumika kutoka mwanzo mwa mchakato huu hadi hapa
ulipofikia hivyo bila msaada wa USD wasingefika hapo walipofika.
“Kuunda
jumuiya na kuisimamia hadi ilipofika hapa sio jambo dogo wangekuwa wananchi
pekee yao wasingefanikiwa kutokana na mchakato huu kuhitaji fedha nyingi sana
na kwa wananchi kingekuwa kitendawili” alisema Kimambo
Kimambo
alisema kuwa WCS ilipita kijiji kimoja hadi kingine kutoa elimu ya uhifadhi wa
wanyama pori ili wananchi wajue umuhimu wa uhifadhi wa wanyapori na ndio maana
kukaundwa hii jumuiya ya WAGA inajumuisha vijiji vitano.
Lakini
Kimambo alivitaja vijiji ambavyo vitanufaika na jumuiya ya hifadhi ya
wanyamapori WAGA ni kijiji cha Nyakadete ambapo ndio makao makuu ya jumuiya
hiyo,kijiji cha Nyamakuyu,kijiji cha Igomaa, Ihanzutwa na kijiji cha Mahoninga.
“Ukiangalia
vijiji hivyo utagundua kuwa vimezunguka katika wilaya kuu tatu ambazo ni wilaya
ya Mufindi,Iringa DC na wilaya ya Mbalali ambapo wilaya hizozipo katika mikoa
miwili ya Iringa na Mbeya” alisema Kimambo
Naye
afisa wanyamapori wilaya ya Mufindi Recho Nambo alisema kuwa katiba ya jumuiya
ya WAGA imetengenezwa kwa mfumo ambao hautasababisha migogoro kama ilivyokuwa
kwenye katiba za jumuiya nyingine.
“Kwa
kweli katika jumuiya hii ya WAGA hatutegemei migogoro tena kwa kuwa tumetengeza
katiba kwa ushirikiano wa wataalam wengi wenye weledi wa maswala ya katiba
hivyo napenda kuwaambia kuwa jumuiya ya WAGA itakuwa ya mfano hapa nchini”
Nambo
No comments:
Post a Comment