Uongozi wa Ubungo Plaza Limited umesema mpangaji wake, hoteli ya Blue Pearl alikoma kulipa kodi ya pango tangu Mei, 2014.
Akizungumza
na waandishi wa habari leo Alhamisi Novemba 9,2017, Ofisa Mtendaji Mkuu
wa Ubungo Plaza, Harun Mgude amesema uamuzi huo umefikiwa baada ya
kushinda kesi Mahakama ya Ardhi.
"Blue
Pearl amekuwa mpangaji wetu tangu mwaka 2006 na mkataba wake ulikuwa wa
miaka 15 ambao ungeisha 2021. Alikuwa akilipa vizuri lakini tangu Mei
2014 aliacha kulipa," amesema Mgude.
Amesema
kutokana hilo walikwenda kufungua kesi Mahakama ya Ardhi na Blue Pearl
wameshindwa, hivyo kutakiwa kulipa au kutoka ndani ya jengo.
"Kama
mnakumbuka tuliwahi kumtoa na akarudi kwa amri ya Mahakama ili kupisha
kesi kuendelea, lakini Novemba 3,2017 kesi iliisha na ameshindwa na
kutakiwa kulipa deni la Sh5.7 bilioni," amesema.
Amesema uongozi wa Blue Pearl umeomba kufanya kikao Jumatatu Novemba 13,2017 ili kujadili jinsi ya kulipa deni hilo.
"Baadhi
ya wateja wamehamishiwa hoteli nyingine sijui ni wapi. Ila ieleweke
kuwa robo tatu ya mali zilizokuwamo Blue Pearl ni za Ubungo Plaza
Limited kama vile fenicha na vitu vingine," amesema Mgude.
Uongozi wa hoteli hiyo ulikuwa ukishughulikia kuwahamisha wateja na haukuwa tayari kuzungumzia suala hilo.
No comments:
Post a Comment