Waziri wa Madini, Angellah Kairuki,
akizungumza na waandishi wa habari kuhusu mafanikio yaliyoanza
kupatikana katika sekta ya madini.
Kairuki alisema serikali itapata mrabaha
wa Dola za Marekani 124,176.97 (Sh. milioni 276.2), pamoja na ada ya
ukaguzi Dola za Marekani 20,695.80 (Sh. milioni 46.036).
Alisema Agosti 31, mwaka huu, serikali
ilizuia mzigo wa almasi za kampuni hiyo zilizokuwa zinasafirishwa kwenda
Antwerp, Ubelgiji na kwamba mzigo huo bado unashikiliwa hadi sasa.
Hata hivyo, alisema serikali iliiruhusu kampuni hiyo kuendelea na uzalishaji wa almasi ambapo na kuzalisha karati 39,567.96.
“Waliomba waruhusiwe kuuza almasi hiyo,
serikali ilikubali na wataalamu wa serikali walithaminisha almasi hizo
na kupata thamani ya awali kuwa ni Sh. bilioni 18.2,” alisema.
Alisema mrabaha wa awali ulilipwa Sh.
bilioni moja na ada ya ukaguzi ilikuwa Sh. milioni 182.2, hivyo serikali
kupata jumla ya Sh. bilioni 1.288.
Waziri Kairuki alisema Oktoba 20, mwaka
huu, almasi hizo zilisafirishwa kwenda Ubelgiji na serikali ilituma
maofisa wake kusimamia uuzwaji wa almasi hiyo ambayo huuzwa kwa njia ya
mnada.
Alisema juzi almasi hizo ziliuzwa kwa
dola za Marekani 10,261,227.76 (Sh. bilioni 22.8) ikiwa ongezeko la Dola
za Marekani 2,069,582.77 (Sh. bilioni 4.6) sawa na asilimia 20.16 ya
thamani ya uthaminishwaji wa awali.
Aliongeza kuwa katika mzigo huo wa
almasi kulikuwa na almasi moja yenye rangi ya pinki yenye uzito wa
karati 5.92 ambayo iliuzwa kwa Dola za Marekani 2,005,555 (Sh. bilioni
4.51).
Aidha, Kairuki alisema Oktoba 29, mwaka
huu, katika eneo la Kiabakari, mkoani Mara, serikali ilikamata sampuli
za miamba ya madini ya dhahabu kilo 600 zilizokuwa zikisafirishwa na
kampuni ya ZEM (T) Ltd bila vibali kutoka serikalini.
Alisema sampuni hizo zilichukuliwa na
kupelekwa kwenye maabara ya Wakala wa Jiolojia Tanzania (GST) na baada
ya kufanyika uchunguzi ilithibitika kuwa kweli ni miamba ya dhahabu.
Waziri Kairuki alisema Serikali imeamua
kuwapeleka mahakamani, ili sheria ichukue mkondo wake kwa kosa la
kusafirisha na kukutwa na sampuli hizo bila kibali.
No comments:
Post a Comment