Mfumuko
wa Bei wa Taifa kwa mwezi Oktoba, 2017 umepungua hadi kufikia asilimia
5.1 ikilinganishwa na asilimia 5.3 ilivyokuwa mwezi Septemba, 2017. Hii
inamaanisha kuwa, kasi ya mabadiliko ya bei za bidhaa na huduma kwa
mwaka ulioishia mwezi Oktoba, 2017 imepungua ikilinganishwa na mwezi
septemba, 2017.
Akizungumza
na waandishi wa habari jana jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi wa
Shughuli za Kitakwimu kwa niaba ya Mkurugenzi Mkuu wa Ofisi ya Taifa ya
Takwimu Bw. Irenius Ruyobya amesema kupungua kwa Mfumuko wa Bei wa mwezi
Oktoba, 2017 kumechangiwa na kupungua kwa bei za baadhi ya bidhaa za
vyakula.
“Kupungua
kwa mfumuko wa bei wa mwezi Oktoba kumechangiwa na kushuka kwa gharama
za baadhi ya bidhaa za vyakula kwa kipindi kilichoishia mwezi Oktoba,
2017 zikilinganishwa na bei za mwezi Oktoba, 2016,” alisema Bw. Ruyobya.
Alitaja
baadhi ya bidhaa za vyakula zilizochangia kupungua kwa mfumuko wa bei
kuwa ni pamoja na unga wa mtama umepungua kwa asilimia 2.6, samaki kwa
asilimia 7.1, matunda kwa asilimia 2.7, mbogamboga kwa asilimia
7.4,maharage kwa asilimia 2.9, viazi kwa asilimia 14.4 na karanga kwa
asilimia 7.8.
Ruyobya
aliongeza kuwa mfumuko wa bei nchini una mwelekeo unaofanana na baadhi
ya nchi nyingine za Afrika Mashariki ambapo nchini Kenya mfumuko wa bei
wa mwezi Oktoba, 2017 umepungua hadi asilimia 5.72 toka asilimia 7.06
mwezi Septemba na nchini Uganda umepungua hadi asilimia 4.8 toka
asilimia 5.3 mwezi Septemba, 2017 Mfumuko wa Bei ambao hupima kiwango
cha kasi ya mabadiliko ya bei za bidhaa na huduma zote zinazotumiwa na
kaya binafsi.
Na Eliphace Marwa, Maelezo
No comments:
Post a Comment