Timu ya Black Sailors “Mabaharia Weusi” wamefanikiwa
kupata alama tatu muhimu kwenye ligi kuu soka ya Zanzibar Kanda ya
Unguja baada ya kuichapa Polisi bao 1-0 kwenye mchezo uliopigwa jioni ya
jana kwenye uwanja wa Amaan.
Bao pekee la Sailors limefungwa na Hassan Said “Kilahe” dakika ya 29 na
kuwafanya sasa wakamate nafasi ya pili kwenye msimamo baada ya
kufikisha alama 12 sawa sawa na JKU ambao pia wana points 12 tofauti ya
mabao ya kushinda na kufungwa huku KVZ wakiongoza ligi hiyo wakiwa na
alama 14.
Saa 8 za mchana Mafunzo wakaichapa KMKM bao 1-0 kwa bao lililofungwa na
Ahmed Maulid dakika ya 28.
Ligi hiyo itaendelea tena kesho kwa kupigwa michezo miwili kati ya
Zimamoto na Jang’ombe Boys saa 8:00 za mchana na saa 10:00 za jioni
Kilimani City watasukumana na Charawe ambayo kwasasa inanolewa na kocha
Ali Bushir.
Na Abubakar Khatib Kisandu, Zanzibar.
Zanzibar 24
No comments:
Post a Comment