Saturday, November 11, 2017

Zanzibar ni sehemu yenye uwezo wa kuzalisha wanafunzi wa zuri


Raisi mstaafu wa Awamu ya sita Amani Abeid karume amezitaka taasisi zenye uwezo kuendelea kujenga vyuo vikuu Zanzibar ili kuwawezesha wananfunzi kujifunza fani mbani mbali katika Nchi yao na kuepukana gharama ya kwenda kusoma nje ya nchi.

Akizungumza katika mahafali ya kwanza kwa wananfunzi Chuo cha ufundi na Biashara Magomeni (Microtech Institute Of Business and Technology ) yaliyofanyika magomeni amesema Zanzibar ni sehemu yenye uwezo wa kuzalisha wanafunzi wa zuri ni ni vyema kwa taasisi hizo kuelekeza nguvu zao katika ujenzi wa vyuo.

Amesema kwa sasa taifa linahitaji wasomi katika kuendeleza maendeleo ya kiuchumi hivyo ni vyema kwa wananfunzi kuendelea kujifunza katika katika nchi  pamoja na kuwa na utamaduni wa kujiendeleza kitaaluma ili waweze kufanya kazi zinazoendana na soko la ajira.

 Kwa upande  Naibu Waziri wa nchi Ofisi ya Makamo wa pili  Raisi Mihayo Juma N’hunga amewataka wahitimu hao kutumia vyema ujuzi walioupata katika  kutumikia taifa pamoja na kuwa na utamaduni wa kujiajiri ili waweze kujikimu kimaisha.

Magazeti ya Tanzania  Leo Jumamos November 11, 2017

Akizungumza na Zenj fm Radio  baada ya Mahafali hayo Mkuu wa Chuo hicho Kamoto Abdul Hassan amesema wataendeleza juhudi zao katika kutoa elimu inayoendana na mahitaji katika soko la ajira ili wanafunzi wanaomaliza waweze kunufaika na elimu wanazopewa vyuoni mwao.

Aidha amesema kutokana na Wananfunzi wa Zanzibar wamekuwa na mwamko mkubwa wa kujifunza fani mbalimbali ni vyema kwa vyuo binafsi kueka ushindani katika kuwapatia wananfunzi elimu bora na inayotambulika wakati wa kutafuta ajira.

Nao wananfunzi waliomaliza masomo yao chuoni hapo wamesema watahakikisha wanatumia vyema mafunzo wanayoyapata katika kutafuta njia za kujiari na kutowa wito kwa wananfunzi wenzao kuachana na tabia ya kusubiri ajira kutoka serikali  jambo ambalo linarejesha nyuma shughuli zao za maendeleo.

Jumla ya wahitimu 157 wamemaliza masomo yao katika chuo hicho wakiwemo wanafunzi Ngazi ya Cheti na Stashahada kwa fani ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano na Ununuzi na Ugavi.

No comments:

Post a Comment