Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akipata maelezo toka viongozi
wa Mamlaka ya Bandari, Jeshi la Polisi na TRA kuhusiana na magari ya
wagonjwa 53 yaliyofichwa katika kona moja ya Bandari ya Dar es salaam
huku wamiliki wake wakiwa hawajulikani alipofanya ziara ya kushtukiza
leo Jumapili Novemba 26, 2017
Rais John Magufuli ametoa siku saba kwa Mamlaka ya Mapato(
TRA), Mamlaka ya Bandari(TPA), Takukuru na Wizara ya Fedha kuhakikisha
inatoa taarifa ni nani alihusika kuagiza magari 50 kupitia mgongo wa
Ofisi ya Rais.
Rais Magufuli ametoa maagizo hayo leo
Jumapili Novemba 26 baada ya kufanya ziara ya ghafla bandarini mara
baada ya kutembelea meli ya Wachina iliyofanya matibabu kwa Watanzania
kwa muda wa siku 5.
Magari hayo aina ya ambulance
ambayo mpaka leo yapo bandarini, yaliagizwa mwaka 2015 kupitia majina
ambayo hayatambuliki na Ofisi ya Rais.
Kabla ya kutoa
maagizo hayo, Rais amewahoji IGP, Waziri wa Fedha, Kamishna Mkuu wa TRA
na Mkurugenzi Mkuu wa Bandari ambao hata hivyo hawakuwa na mujibu kuhusu
nani hasa mwagizaji wa magari hayo.
"Natoa onyo kwa
mawaziri na wateule wale wote waliotangaza, sitaki mpaka nije kubaini
uozo mimi mwenyewe ninataka mpigane kuhakikisha uozo wote unaondoka,
safari nyingine nikigundua jambo lolote na wewe ni eneo lako hautapona,"
amesema.
Ameongeza, "Ninatoa siku saba, nataka
aliyeagiza haya magari kwa mgongo wa Ofisi ya Rais atambulike ni nani na
ninatoa maagizo hata kama ni mtu mkubwa kiasi gani atambulike nahitaji
mujibu."
Wakati huohuo Rais Magufuli ametembea umbali
wa zaidi ya mita 700 ili kukagua magari ya polisi ambayo yaliingizwa
nchini mwaka 2015 lakini bado zaidi ya magari 50 yameendelea kubaki eneo
la bandari.
Amemwagiza IGP kuhakikisha anayakagua magari hayo na kuyatoa bandarini ili yakafanye kazi ambayo ilikusudiwa.
"Kwa nini magari yanakuja hapa yanakaa miaka 10, wakati sheria inasema ni siku 21? Amehoji Rais Magufuli.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akipata maelezo toka viongozi
wa Mamlaka ya Bandari, Jeshi la Polisi na TRA kuhusiana na magari ya
wagonjwa 53 yaliyofichwa katika kona moja ya Bandari ya Dar es salaam
huku wamiliki wake wakiwa hawajulikani alipofanya ziara ya kushtukiza
leo Jumapili Novemba 26, 2017
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akikagua sehemu ya magari zaidi
ya 6000 yaliyopo bandari ya Dar es salaam mengine yakiwa hapo kwa miaka
zaidi ya kumi bila kuchukuliwa na wenye nayo alipofanya ziara ya
kushtukiza leo Jumapili Novemba 26, 2017

Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akitoa
maelekezo kuhusu magari zaidi ya 50 ya Jeshi la Polisi yaliyopo
bandarini toka mwaka 2015 kwa sababu ya kutolipiwa ushuru alipofanya
ziara ya kushtukiza leo Jumapili Novemba 26, 2017

PICHA NA IKULU
No comments:
Post a Comment