Chama Cha Mapinduzi leo kimehitimisha kampeni zake za uchaguzi mdogo katika kata ya Mhandu Jimbo la Nyamagana mkoa wa Mwanza
Akizungumza katika kuhitimisha kampeni hizo Mbunge wa Jimbo la Ilemela Mhe Dkt Angeline Mabula amewataka wananchi wa kata ya Mhandu kujitokeza kupiga kura na kumchagua mgombea udiwani kwa tiketi ya CCM ndugu SIMA CONSTANTINE SIMA kuwa diwani wao siku ya kesho kwa kuwa ndie mtu sahihi katika kujiletea maendeleo huku akiwaelezea juu ya hatua zilizochukuliwa katika kutatua changamoto za ardhi
Kwa upande wake Mbunge wa Jimbo la Bukombe Mhe Doto Biteko amewaasa wananchi hao kumpa Kura za Ndio mgombea huyo na msomi anayetambua masuala ya uchumi kunakomfanya kuwa mtu sahihi katika kuyafikia malengo ya Serikali ya kuwa na nchi ya Uchumi wa kati kupitia uwekezaji katika sekta ya viwanda huku akiwashangaa wapinzani kwa kitendo chao cha kupotosha umma cha kusema kuwa hakuna utekelezaji wowote wa shughuli za maendeleo
Nae Mbunge wa Jimbo la Nzega mjini Mhe Hussein Bashe mbali na kuelezea juu ya historia ya kuanzishwa kwa mfumo wa vyama vingi kuto jaribu tena wapinzani kwa kuwapa madaraka huku akiwakumbushia historia ya miaka kadhaa iliyopita ya kipindi cha kutawaliwa na upinzani na kusababisha kusimama kwa shughuli za maendeleo sanjari na kuwaambia kuwa mabadiliko ya kweli yataletwa na chama cha mapinduzi nasi vinginevyo
Mgeni rasmi wa mkutano huo wa hadahara alikuwa mjumbe wa kamati kuu ya CCM Mhe Stephen Wasira huku viongozi wengine mbalimbali wakihudhuria akiwemo Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Mwanza Antony Dialo, Katibu wa CCM mkoa Mwanza Mwalimu Raymond, Mbunge wa viti maalumu kupitia kundi la wanawake wa mkoa Mwanza, Mkuu wa wilaya ya Nyamagana Mhe Mary Tesha, Mbunge wa Jimbo la Nyamagana Stanslaus Mabula, Mstahiki Meya wa Jiji la Mwanza Mhe James Bwire, Aliyekuwa mwenyekiti wa BAVICHA Patrobas Katambi, Aliyewahi kuwa Waziri wa mambo ya ndani ya nchi Mhe Lawrence Masha, Madiwani, Wajumbe wa Kamati za siasa za wilaya ya Nyamagana na Ilemela na Dk SHIKA
' Ilemela ni yetu, tushirikiane kuijenga '
Imetolewa na
Ofisi ya Mbunge
Jimbo la Ilemela
25.11.2017
No comments:
Post a Comment